Simba SC nawaomba Okra awe anaanza Kikosi cha Kwanza na Sakho atokee Benchi au hata asipangwe kabisa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama kuna Mchezaji wa Simba SC ambaye Kutwa anatupandisha Hasira wana Simba SC na hatujui ni kwanini Makocha huwa wanapenda Kumuanzisha First Eleven ni huyu Pape Ousmane Sakho.

Na kama kuna Mchezaji ambaye Simba SC ni muhimu, tegemeo na Lulu Kwetu kutokana na Kipaji chake Tukuka ( tena kumzidi hata Sakho ), ila hatutaki Kumuamini na Kumtumia vyema ni huyu Kiungo Mshambuliaji Augustine Okra.

Ni kweli nakiri na kutaarifiwa na Mmoja wa Mdau wa Soka aishiye nchini Ghana kuwa Okra hawezi Kucheza dakika zote 90 na anaweza tu Kucheza dakika 75 ila zinafaida kuliko dakika zote 90 ambazo Sakho anazicheza huku akiwa anarukaruka tu Uwanjani na kutafuna hovyo Bubble Gum ( Big G ) na mdomo wake ulio kama Chuchunge vile.

Okra awe anaanza badala ya Sakho na hapa hata tusiwe Wanafiki Simba SC ya jana bila kuingia kwa Okra na vile alivyokuwa akicheza, akiwakimbiza Mabeki huku akipiga Miwa ( Mashuti ) ya maana tungeishia kutoka Suluhu na kuendelea Kuuimba Wimbo wetu mpya na pendwa wa "Hatumtaki Matola" na jana huenda ingekuwa ni Remix yake.

Tafadhali sana Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally nimedokezwa na Mdau wako Mmoja kutoka Azam Media ulikokuwa kuwa huwa Unanisoma mno hapa JamiiForums na MImi GENTAMYCINE ni Follower wako basi nakuomba nifikishie hili kwa akina Mgunda, Matola na Rweymamu na lifanyiwe Kazi haraka.
 
Sakho si ndie yule wa Magoli ya CAF Sasa itakuaje akianzia Bench? Sakho ana fanana na winga wa Zamani wa Simba Sunday Juma, mda mwingi anataka kukimbia na mpira tofautiyao Sunday alikua akipiga Kross akifika kwenye kibendela Cha Kona ila Sakho anapenda kukimbia katikati ya Difensi kitu kigumu Kwa mpira wa kisasa. Angekua ana achia haraka na kuomba Tena angekua mzuri sana.
 
Phiri na Okrah pesa za Simba zimeenda kihalali kabisa.Sakho ni mzuri sana kwenye kupaka poda mpira ila kupambana hawezi kwanza mwepesi kuumia.
 
Sakho anataka mechi zenye mauzo kama club bingwa na Shirikisho ,Kwa Sasa Sakho ataki kuumizwa Kwa Kupigwa makwanja yasiyo na sababu,Sakho awezi kuangaika dhidi ya prison akaumizwe ,alifanya hivyo mechi ya biashara akapigwa makwanja mpaka penalty ikapatikana Boko akakosa, kaumia miezi mitano ,yote hayo ya Nini?atasubiri kucheza na wanaojua mpira na Simba itajipatia Pesa ya kutosha kupitia Sakho
 
Kwa hiyo sakho anaweza Moira wa kujiburudisha wakati sisi tunataka kamba
 
Kama kuna Mchezaji wa Simba SC ambaye Kutwa anatupandisha Hasira wana Simba SC na hatujui ni kwanini Makocha huwa wanapenda Kumuanzisha First Eleven ni huyu Pape Ousmane Sakho.

Na kama kuna Mchezaji ambaye Simba SC ni muhimu, tegemeo na Lulu Kwetu kutokana na Kipaji chake Tukuka ( tena kumzidi hata Sakho ), ila hatutaki Kumuamini na Kumtumia vyema ni huyu Kiungo Mshambuliaji Augustine Okra.

Ni kweli nakiri na kutaarifiwa na Mmoja wa Mdau wa Soka aishiye nchini Ghana kuwa Okra hawezi Kucheza dakika zote 90 na anaweza tu Kucheza dakika 75 ila zinafaida kuliko dakika zote 90 ambazo Sakho anazicheza huku akiwa anarukaruka tu Uwanjani na kutafuna hovyo Bubble Gum ( Big G ) na mdomo wake ulio kama Chuchunge vile.

Okra awe anaanza badala ya Sakho na hapa hata tusiwe Wanafiki Simba SC ya jana bila kuingia kwa Okra na vile alivyokuwa akicheza, akiwakimbiza Mabeki huku akipiga Miwa ( Mashuti ) ya maana tungeishia kutoka Suluhu na kuendelea Kuuimba Wimbo wetu mpya na pendwa wa "Hatumtaki Matola" na jana huenda ingekuwa ni Remix yake.

Tafadhali sana Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally nimedokezwa na Mdau wako Mmoja kutoka Azam Media ulikokuwa kuwa huwa Unanisoma mno hapa JamiiForums na MImi GENTAMYCINE ni Follower wako basi nakuomba nifikishie hili kwa akina Mgunda, Matola na Rweymamu na lifanyiwe Kazi haraka.
we yanga damu,Mambo ya Simba yanakuhusu Nini kijana, we si kutwa unaisema Simba vibaya, juzi tu umehaidi utaishambulia kwa kuichafua simba Hadi mwisho wa msimu,
Jitaidi huwe unakunywa vidonge vyako kwa ufasaha
 
Tafadhali nakuomba uweke hapa Ushahidi wa huo Uzi ambao Mimi GENTAMYCINE na hii ID yangu pekee hapa JamiiForums nimesema hivyo.

Nasubiria .....!!!!!!
 
Back
Top Bottom