Kong xin cai
Member
- Dec 12, 2020
- 76
- 87
Ni masaa kadhaa tangu shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF kutoa taarifa rasmi ya kuahirishwa kwa mchezo na 178 wa ligi kuu Tanzania bara huku mashabiki na wadau wa soka nchini wakiachwa vinywa wazi. Taarifa hii imekuja mara baada ya timu Simba Sc ikidai kuzuiwa kufanya mazoezi yao ya mwisho ya kujiandaa na mchezo wao wa dabi dhidi ya timu ya yangu. Tukio hilo lilitokea majira ya saa moja usiku katika geti la kuingilia uwanja wa Benjamin mkapa, ambapo wanaosemekana kuwa ni walinzi wa klabu ya yanga walizuia mabasi ya klabu ya simba kuingia ndani ya uwanja hali iliyopelekea simba sc kuiandikia barua kamati ya utendajia na usimamiza ya michezo TFF kutoridhishwa na kitendo hicho.
Mapema hii leo, TFF walitoa tamko kuwa timu yoyote ambayo hatofika uwanjani itapigwa na faini na adhabu mbalimbali kama ambvyo sheria za mpira wa miguu zinavyosema, lakini mda mfupi baadae walikuja kutoa taaifa nyingine inayohararisha kuahirishwa kwa mchezo huu.
Klabu ya Simba imefanikiwa, kwa kutumia falsafa ya mwenekiti wa chama cha upinzani kwa "pasipo mabadiliko a kiutendaji na usimamizi wa sheria, hakuna uchaguzi"
INEC, TFF na taasisi zingine za umma, msisubiri mpaka siku wananchi wenyewe wataposimame kudai haki zao, simamieni sheria zenu kwa usawa bila kuingilia au kuwanyima nafasi upande mwingine. Tupo kwenye nyakati za mabadiliko