Simba SC Tanzania: Taarifa kwa vyombo vya habari

Simba SC Tanzania: Taarifa kwa vyombo vya habari

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
835
Reaction score
1,608
SIMBA SPORTS CLUB
D'SALAAM, TANZANIA
14/12/2016


*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*.

Klabu ya Simba inapenda kutangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog.

kwenye maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu

Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, pamoja na Emmanue Semwanza atakaekwenda Maji Maji fc ya Songea,

Huku pia klabu ikiachana rasmi na Golikipa muaivory coast Vicent Agban na kiungo Mcongo,Mussa Ndusha.

Sambamba na kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James kotei, huku tukikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma luizio anayekuja kwa mkopo toka Zesco ya Zambia.

Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Alli kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta kwetu kwa mkopo.

Tunaamini maboresho haya yataongeza chachu ya ushindani ktk kikosi chetu na Hatimaye kutupa mataji msimu huu.

Niwaarifu pia timu yetu imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda Fc, mchezo utakaopigwa siku ya jumapili ya tarehe 18/12/2016 huko Mtwara.

Imetolewa na ;

*Haji S. Manara*
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sc

*SIMBA NGUVU MOJA*
 
Kwani yeye haujui kuandika????! Acheni dharau nyie wa upande Wa pembeni jirani
 
Makosa sana kumuachia kipa mtakuja kujuta naawaambia
Kama kocha bora kabisa kwa sasa katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, Omog.. Ambae amekaa na Angban kuanzia katika mazoezi daily hadi kwenye mechi, kasema Noooo.. Kwann wewe useme Yes??
Angban alikua na mapungufu lukuki, japo ndo hivyo tulikua tunamezea.. Zile mechi kibwena alizocheza bila kufungwa zisikutushe, jamaa alikua anabebwa na uimara wa beki tu.
 
Ameandikiwa nananii hivii
Jifunze kuandika kwanza ndio ukosoe wengine.Toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kuona ubanzi kwenye jicho la mwenzako. Nobody is perfect.
 
Kama kocha bora kabisa kwa sasa katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati, Omog.. Ambae amekaa na Angban kuanzia katika mazoezi daily hadi kwenye mechi, kasema Noooo.. Kwann wewe useme Yes??
Angban alikua na mapungufu lukuki, japo ndo hivyo tulikua tunamezea.. Zile mechi kibwena alizocheza bila kufungwa zisikutushe, jamaa alikua anabebwa na uimara wa beki tu.
Kama Angban angecheza ligi ngumu zenye washambuliaji wakali,angeishafikuzwa.Jiulize mbona Ngoma na Tambwe walikuwa wanamfunga kila mechi wakikutana na Simba.
 
Aghban kawanyima ubingwa last year mkabaki Yanga inabebwa. Agban alipaswa kusogea acheze mpira aliorudishiwa na Kessi akaganda golini
 
simba kweli mtakuja kuchukua ubingwa kwa wachezaj wa mkopo?hili nalo jipu la kutegemea wachezaj wa mkopo.
 
Back
Top Bottom