Simba SC: Tulikuwa na nia kumwacha Thadeo Lwanga sababu ya majeraha. This is foolish!

Action and Reaction

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2021
Posts
1,438
Reaction score
1,496
Thadeo Lwanga ilikuwa tusitishe mkataba wake mwezi huu kutokana na jeraha lake kuchelewa kupona na tulikuwa tayari kutafuta mbadala wake ila daktari ametuhakikishia atakuwa amepona kufikia mwisho wa mwezi huu (January)” amesema Ahmed Ally.

Yaani wenzenu wanapeleka wachezaji wao kutibiwa nchi za nje kwa gharam kubwa.... nyie mnawatema, kweli timu yangu haiwajali wachezaji wake Wanawashinda Azam na Yanga aisee!

Kwahiyo huyo Kanote ndo mbadala wa Lyanga, haingii hata nusu, kazi kupepesuka miguu tyu! Nasema Kanote tumepigwa....... yaani anashindwa na Mkude daaa!

Manara alikuwa sahihi kusema "timu inaacha wachezaji wake wazuri kisa majeraha"
 
Ni ujinga kutema mchezaji mzuri kisa majeruhi.
 
Hii habari nimeiona Jana nikaipuuza. Lakini sasa naanza kuamini Ahmed Ally ni kimeo. Jambo kama hili hata kama lipo unaliacha jikoni siyo la kutoa nje maana linaharibu image ya timu. Hivi wachezaji wanajisikiaje wakisikia wanaachwa kwenye usajili mara tu wanapoumia?
 

Mkuu sio hilo tuu na Kulogana Kupo hapo ....Unaweza Kulogwa ukawa Hupangwi au Majeruhi au Huelwani na Coach...Wapunguze Tuu Uchawi[emoji3516][emoji12][emoji12]
 
Niwe muwazi sina imani na Simba yangu hivi karibuni ikiwezekana hata Matola atafutiwe nafasi nyingine kama wanaogopa kumfukuza, Mseng* ni kimeo yule

Unamaanisha anashirikiana na wale wazembe wa ndani kupewa kidogo na kuloga wachezaji haswa wa Nje?[emoji30][emoji30][emoji30]
 
Sasa mkuu unataka kusema Mkude ni mchawi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…