Simba Sc tumemsajili kiungo wa Ivory Coast, Ahoua Jean

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Klabu ya Simba tumethibitisha kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast 🇨🇮 kwa mkataba wa miaka miwili.

Ahoua mwenye umri wa miaka 22 amesajiliwa kutoka klabu ya Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast.

Katika msimu wa 2023/24 Ahoua ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa.

Ahoua anasifika kwa kufunga mabao kutoka umbali mrefu, kuchezesha timu pamoja kutengeneza nafasi kwa wenzie.

PIA SOMA
- Ahoua Jean Charles usajili bora zaidi Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…