Simba SC tunakwama wapi?

Joined
Nov 21, 2018
Posts
29
Reaction score
26
Simba sasa tumekuwa kama pombe ya ngomani kila mtu anataka ainywe.

Hakuna timu sasa inayoogopa kucheza na Simba. Inashangaza sana kuona timu zinafunguka mbele ya Simba wakati nakumbuka ukiwa unacheza na simba lazima uchague kati ya haya ufunguke upigwe Mkono au ujilinde upigwe 2 au tatu.

Hali sasa imekuwa tofauti kabisa timu zinafunguka zinaweka mpira chini mpaka wakati mwingine mimi mshabiki wa Simba naombea Mpira uishe. Anzia match na Makwasukwasu fc kwa kweli nilikuwa naomba mpira uishe.

Njoo kwa Polis JKT pamoja na kwamba tulishinda ila polis waliupiga mwingi sana. JKT leo wakutufunga jamani.

Tuachane na Hayo.

Nini cha kufanya viongozi wa Simba
Kwanza kabisa viongozi wa simba wajitadhmini na wajichunguze nahisi wengi wao wapo ki maslahi. Huwa najaribu kujiuliza kosa la uchebe lilikuwa haliwezi kuvumilika na kurekebishika? Uchebe Alikwama wapi? Binafsi uchebe alikwamishwa na viongozi wenye kupenda matumbo yao. Kwanza wachezaji aliowaomba haukupewa na aliowaomba wabaki pia uongozi uliwaacha wakaondoka sasa unasajili wachezaji kwa matako yako wewe kiongozi.

Kocha aletwe mwingine na kuhusu kusajili akabidhiwe kocha pia. Mo kwanini swala la wapiga dili usiachane nao? unarudisha mizigo ile ile kwenye uongozi fukuza wote tia pesa yako jenga heshima kwanza Africa kwa kuchukua hata kombe mara moja. Ndio maana hata timu ndogo ikipangwa na Simba hawaogopi tena Ila ukichukua champion league timu itakuwa na hofu na wewe.

Kwa heri. Mo zingatia ushauri huo
 
Simba walikosea kwenye usajili wamemuuza kotei Hadi sasa hiv pengo lake linaonekana kotei alikuwa mnyama ana nguvu anakaba kwelikweli aliziba udhaifu wa mabeki wa Simba ukiangalia kwa team ya Simba ya sasa mtu Kama huyu hawana.Kiufupi team aipo balance wanawachezaji wengi wakuchezea mpira wakabaji hawana mkude na fraga sio defensive midfielders Bali both ni holding midfielders.

Kosa lingine ni kumuuza okwi bila kuleta mtu sahihi wakuziba pengo lake Kama Kagere akiwa afungi okwi anatupia mpaka okwi anaondoka alikuwa mfungaji wa pili wa Vodacom premier league viongozi wa Simba wakamleta yule striker garasa wa kibrazili.Kingine msimu uliopita Simba walikuwa na tatizo la mabeki nilitegemea wakamleta mtu sahihi Kuna yule beki number 5 wa nkana ni bonge la beki lakini hajamsajili wameleta magarasa.

Kosa lingine ni kumfukuza uchebe ambaye alishatengeneza team vizuri na ameipa Simba Mafanikio makubwa msimu uliopita na mpaka anaondoka Simba ilikuwa inaongoza league na team inacheza vizuri kwa miemuko ya uongozi wakamfukuza kazi badala yake wameleta kocha garasa.


NB: Mpira wa Tanzania una haribiwa na vingozi Mara nyingi kwa maamuzi mabovu wanayofanya kwa kutofuata uweredi kwenye utendaji wao.
 
Freshi tu
TUFANANE!

kelphin kepph
 
Safi sana Innocent kwakweli yule beki wa nkana alikuwa kisiki kweli kweli. Pengo la simba champion league ilikuwa ni mabeki haswa beki ya kati na mabeki wa pembeni maana mipira ya juu na kona mabeki walikuwa wafupi na ndio maana tulikuwa tunafungwa magoli ya ajabu na pia uzembe wa kutokuruka kwao. Kwa sasa simba wajitaidi kuangalia ni nani atakaye tusaidie kwenye champion league kama tutachukua ubingwa. tuongeze mshambuliaji mmoja mkali na msumbufu kiungo zaidi ya kotei na mabeki wawili naimani tunaweza kuongea lugha moja kwenye champion league.
 
Tungeweza Kumchukua Pierre Lechantre Kwa kweli nilimwona kama kocha mzuri sana na kama Uongozi wa simba mnaweza komaeni na yeye Japo story za vijiweni Nasikia mnamfikiria yule kocha wa AS Vita ya Kongo. Binafsi namwona ka ma kocha mzuri ila kuna kaugumu kidogo kuiacha timu ya Congo. Na nasikia anatka mupesa mingi M90. Wakati Lechantre alikuwa anataka M50 Kwa tetesi za watu wa karibu.
 
Tatizo la lenchantre soka lake lilikuwa halivutii natulikuwa tunapata ushindi kidunchu
 
Kiukweli Simba Imefanya Usajili wa Ovyo Sana Msimu huu, badala ya Kuimarisha kikosi Wao wakakibomoa kile kikosi kilikua kihitaji marekebisho kidogo tu, hasa kwenye Safu ya Ulinzi

Uamuzi wa Kumfukuza Uchebe ulikua Wa Ovyo Sana Kuna Viongozi Pale Simba ni Wapiga dili,.

Pesa Za Mo Zinatumika Vibaya sana Pale Simba hakukua Na haja Ya Kumrudisha Kichuya wakati una matatizo ya beki
 
Aliyetupiga tano alipata faida gani kwa kuwa nasi tulimpiga na tukamtoa? Ni sawa na wewe umelala na mke wa mtu usiku kucha umefanya unayoyajua asubuh karudi kwa mume wake mume kuja kujua naye kalipiza kibao kwa mke wako ila yeye hakulala naye bali aligonga hodi mara mbili then akamwachia mkewo kumbe mkeo alikuwa kwenye danger days matokeo yake kanasa halafu jioni yake unaenda kula mzigo kama kawaida mtoto anazaliwa sio wa kwako. hicho ndicho walichokifanya AS VITA CLUB YA CONGO
 
wapiga dili ndio wanamuweka Mo mikiani..akiwavuruga anafukuzwa wataungana na yule mzee wa Kinondoni
 
Mnaniboa sana mnapozungumza ooh Kotei ooh Uchebe, come on lets move on!! You know kwamba hao wameshapita Simba.

Ni sawa na mie nianze kuwakumbuka akina Lilla Shomari, Mtemi Ramadhani, they are long since gone focus on the present time and going forward please!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi bado kuna watu wanaamini kwa kocha huyu huyu Sven Simba itatwaa ubingwa wa ligi? Hivi wale wajumbe wa bodi ya Simba waliokuwa wanapitapita kwenye vyombo vya habari kumsema vibaya Uchebe wapo wapi sasa hivi? Kidogo nilimsikia mmoja juzi akiwatupia lawama wachezaji na kumtetea Sven eti wachezaji wanacheza chini ya kiwango ili kocha atimuliwe.

Kumfukuza Uchebe halikuwa tatizo kwa sababu viongozi wao ndio wanajua kwa nini walifanya maamuzi hayo ila je umemleta nani kuchukua nafasi yake? Tutakatae tukubali Sven sio kocha wa kiwango cha kufundisha Simba. Kwa kikosi kilichopo Simba inahitajika tu kuisoma timu pinzani na mfumo inaotumia basi wewe unapanga kikosi chako na mbinu zako kwa sababu Simba ina mseto wa wachezaji wenye vipaji tofauti tofauti wanoweza kukupa matokeo katika mifumo tofauti tofauti. Kwa ligi ya ndani bado kikosi cha Simba kinaweza kushindana na kutetea ubingwa iwapo kikipata kocha mzuri.

Sven mfumo wake wa kutumia mshambuliaji mmoja badala ya wawili huwa unazipa sana nguvu timu pinzani kwani zikishamkamata Kagere au Boko basi biashara imeisha. Kagere sio aina ya washambuliaji ambao unaweza kumtumia katika mfumo wa mshambuliaji mmoja kwa sababu hana kasi sana na sio mzuri sana wa kukaa na mpira mguuni. Hili Profesa Uchebe alilijua ndio sababu kubwa alikua anaanza na Boko na Kagere pamoja kwa vyovyote timu pinzani lazima ibaki nyuma kujilinda na hivyo ilikuwa inawapa nafuu viungo na mabeki wa Simba. Ndio maana mapungufu ya ukuta wa Simba yameonekana sana sasa hivi wakati yalikuwepo tangu msimu unaanza. Sasa kwa kocha wa kiwango cha Sven hata hili dogo linamshinda kuona vipi kwa mbinu nyingine za kimchezo ataweza kweli?

Mapungufu mengine makubwa kwa Sven ni kuwa hajui kupanga kikosi kwa ufanisi kulingana na ukubwa au aina ya mechi. Upangaji wake ni kama anapiga ramli. Pili si mwepesi wa kufanya "sub" kwa wakati na hata wakati mwingine akifanya hizo "sub" anazidi kuingamiza timu badala ya kuisaidia timu.

Na sasa hivi hatulalamiki tu Simba kufungwa bali hata kiwango cha timu kimekuwa cha kawaida sana. Simba ya sasa haitishi ndio sababu timu yoyote inayokuja uwanja wa Taifa inafunguka na kama haujui rangi ya jezi si rahisi uitofautishe Simba na timu pinzani kwa kiwango chake. Mpaka unajiuliza ndio uwanja huu huu Alhaly, As Vita, Soura, Nkana na wengineo walifia hapa?

Kutegemea Sven atetee ubingwa hizi ni ndoto za mchana kwa sababu hata mfumo unaompa manufaa yeye mwenye hauamini. Siku zote anaanza na mshambuliaji mmoja timu inafungwa anaingiza mshambuliaji mwingine timu inakuwa na washambuliaji wawili wanakomboa goli na kuongeza goli lingine. Kwa kuwa ni sikio la kufa mechi ijayo badala aanze alipoishia anarudi tena anaanza na mshambuliaji mmoja. Kwangu mimi huyu alipaswa kufukuzwa mara moja kwa sababu mechi kuanzia ya Mwadui, Namungo na Polisi kiukweli timu ilicheza vibaya sana kama vile haina kocha na ni kama tulifungwa tu zile mechi sasa sijui viongozi wanasubiri nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…