chibuOG
Senior Member
- Apr 11, 2024
- 169
- 337
Simba Sports Club pamoja nakuwa na kundi kubwa la wachezaji wapya pamoja na benchi la ufundi jipya kabisa lakini bado wameonyesha kuwa wao ni timu namba moja kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Namba 6 kwa ubora kwa vilabu Afrika nzima.Yaani ule mpira waliocheza jana ndio huwa unampa ubingwa Al Ahly ya Misri,Unacheza kwa malengo sio tu ilimradi na kiwango kile naiona Simba ikifika mbali sana tena ikiwezekana hata kombe watachukua.
Halafu mnaombeza Fadlu Davis kwa kumuacha nje Mukwala na kumuingiza Valentino Mashaka naomba niwaambie ukocha ni taaluma na watu wanasomea kwahiyo muacheni Mtaalamu Fadlu afanye majukumu yake kwa taaluma yake.