Simba SC wamechea kikubwa na kimkakati

Duu hata kama mwalimu anakosea basi nasisi tukosee yaani tufikirie anavyotaka yeye, mnanikumbusha zidumu fikra za..............
 
Mpira wa kushindwa kupiga hata pasi 7 kwa usahihi?
Mpira wa kushambuliwa mwanzo mwisho?
Mpira wa kushindwa hata kutengeneza nafasi?
Mpira wa kushindwa kupata hata on target moja?
Wachezaji hata unyumbulivu hawana?
Nyie Utopolo mlipata nafasi ngapi..mkafunga goli ngapi?!
 
Kweli kabisa hata walivyokuwa wanapoteza pasi kizembe ulikuwa mkakati
 
Uto pole mtani! nyie mmetolewa jasho na katimu kabovu kasikokuwa hata na mashabiki!!
 
Mnamsikiliza Ahmed Ally ambaye anawapamba na kuwapa moyo tu na inaonekana siyo mtu wa mpira kabisa.

Sare ambayo ingekuwa nzuri ni ya MAGOLI.

Sare ya bila goli ni mbaya Sana maana Al Ahly wakipata sare yoyote ya magoli kwa Mkapa, Simba OUT.

Na ukiona Simba ilivyocheza na Al hilal (Sudan) na Al Ahly Tripoli inaonesha ni timu ya pili.

Kwa vyovyote hata kwa Mkapa Simba itakaa nyuma ya mpira, kulinda. Mijamaa ya Tripoli inakaba, inakimbia kinoma.

Aliyewadanganya Simba ni vijana ma Tripoli ni wazee awaombe msamaha
 
Simba hata ikikaa nyuma LUPASO bado itashinda hiyo mechi ndani ya dakika 90 wala Al Ahly hawatapata hiyo sare unayoombea itokee ili uje useme Si niliwaambia? Inshaallah Simba itashinda kwasababu tuna silaha hatukuzitumia kabisa away kama AWESU AWESU na MUKWALA kwahiyo mechi ya Marudiano ni mechi nyingine kabisa kiufundi na kimbinu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…