Kupitia ukurasa wa Mtandao wa Instagram ya timu ya Simba sports club wameandika kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa kitita cha Millioni 15 kama zawadi kwa mabao matatu waliyofunga timu ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini
"Asante Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa zawadi ya Tsh. 15,000,000 kama zawadi ya mabao matatu tuliyowafunga Nsingizini Hotspurs" - wameandika Simba sports club
Fedha hizo zilikabidhiwa na Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kwa Mkurugenzi wa Bodi Cricentus Magori pamoja na nahodha wa Simba Shomari Kapombe
Matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi huku zikiwa na dalili zote za rushwa! Na hii siyo kwa simba tu! Hata zikitolewa kwa Yanga, SBS, Azam, nk. Haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
Hilo mnaloita goli la mama ni ujinga na upumbavu michezoni. Hakuna team inayohitaji hizo pesa kujiendesha ila tu ni siasa michezoni na mnajua athari zake so nyie wana habari na vyombo vyenu acheni huo upumbavu wa kutumika kisa njaa zenu. Acheni football isimame kwenye misingi yake, yeye kama anazo hizo pesa apeleke mahospitalini huko ambako wananchi wanakufa kwa kukosa huduma au mashuleni ambako watoto wanakaa chini au kusomea chini ya miti. Kama zipo za kutosha awalipie Bima watoto wa masikini wanaohangaika na wazazi wao kutafuta matibabu baada ya kuwafutia Bima ya watoto. Kataeni siasa michezoni.