Simba SC wanaenda kuharibu

Simba SC wanaenda kuharibu

Naona mapigano 5,7 , nk sasa hofu ya nini? Uliyaona magoli ya muamala ya prisons?
Ahaaa ,we hukumuona yule asukile analia kukosa milioni za gsm,hukumuona kipa wa prison alivyopangua mikwaju ya saidoo.
Referee alikuwa fair sana kawanyima simba penati mbili
 
Ahaaa ,we hukumuona yule asukile analia kukosa milioni za gsm,hukumuona kipa wa prison alivyopangua mikwaju ya saidoo.
Referee alikuwa fair sana kawanyima simba penati mbili
Nitakuwekea hapa goli beki anampasia boko afunge. Pure tiGO Pesa
 
Mi pia naimani sana na Mgunda

Mechi tulizo poteza au kushindwa kupata alama 3 kulichangiwa na ukosefu wa Quality players ulio wataja

Sijaona mechi ambayo tumefanya vibaya halafu tatizo likaonekana ni kocha

Anyway ngoja ruone itavyo kuwa
 
Habari wanamichezo.

Hivi karibuni zimeibuka tetesi Simba SC wanahitaji kuajiri kocha mkuu na kocha anaepewa nafasi kubwa ni yule Mbrazil wa Vipers.

Kwa mtazamo wangu naona Simba SC wanajiandaa kuivuruga timu na kuanza moja.

Kuhitaji kocha mpya kwa sasa huku timu ikiwa kwenye mbio za ubingwa ni kurudisha nyuma maendeleo ya timu hasa kiuchezaji, bado siku 40+ michuano ya klabu bingwa ianze je Simba SC wanatarajia nini?

Ikumbukwe ujio wa kocha mpya kwa sasa kunaweza kuathiri viwango vya baadhi ya wachezaji hivyo kupelekea timu kufeli kufikia malengo.

Kocha Mgunda anatosha vyema, kinachotakiwa kwa sasa Simba ni kujaza nafasi walizo puyanga katika usajili wa dirisha kubwa. Kikosi cha Simba kimekosa Mshambuliaji mahiri na kiungo mkabaji mahiri.

Wachezaji hawa walikuja kujaza nafasi tu ila viwango vyao ni vya kawaida.

1. Dejan (Mshambuliaji) ameshaondoka.
2. Outtara (beki wa kati)
3. Nelson Okwa (Kiungo mshambuliaji)
4. Victor Akpan (Kiungo mkabaji) usajili mbovu kabisa (uwezo anazidiwa na Majogoro)

Iwapo Simba SC itasajili wachezaji wa viwango vya juu kuziba nafasi hizo 4 ambapo nafasi moja tayari Ntibazonkiza ameshasajiliwa basi haina haja ya kocha mpya.

Watu wanaohusika kwenye usajili watazame pia nafasi hizi:-

1. Beki wa kulia (Kapombe hana mbadala sahihi)

2. Beki wa kushoto (Gadiel Michael uwezo wake umeshuka)

3. Beki wa Kati (Onyango sio kuaminika sana, Kennedy amefeli kushindana na Onyango)

4. Kiungo Mkabaji wa viwango vya CAF (hizi tetesi za kutaka kumsajili Nashon wa Geita Gold naona Simba hawapo siriazi kabisa)

Mgunda akipewa wachezaji sahihi na imani ataifikisha timu mbali.

Kama ni habari za kocha mpya, subirini msimu uishe ndiyo muajiri kocha mpya lakini pia aje na wasaidizi wake.
Maana yake unataka Simba isajili wachezaji wapya wa kigeni wanne na iachanae na wachezaji wengine wanne wa kigeni?
 
Hatumtaki nchini aende hata china huko kwani lazima achezee bongo,yule ndio anafanya simba ionekane mbovu,nina imani hata kocha nabi anamshukuru sana ,
Anatakiwa kuvunjwa mguu au atafute nchi ya kuchezea
Mkuuu ana familia ujuee😆 😆 😆
 
Nailaumu bodi ya wakurugenzi kwa maamuzi waliyo yafanya, wameigharimu timu pakubwa.
 
Pesa za kuahidi bonasi milioni 300 mnashindwa kusajili wachezaji wa maana mnaenda kuokota mchezaji amekaa miezi zaidi ya 8 hajacheza mechi.

Sasa tunafurahia kupiga pasi ila matokeo yamekua adimu.
 
Back
Top Bottom