Simba SC Wanakwama Wapi?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Ngoja tuzungumze kitu.

Kwanini mtani umeshindwa kumuiga Bingwa wa mara zote wa Ligi Kuu linapokuja suala la "Players recruitment"?. Haiwezekani kilaa dirisha la usajili wewe unaacha kundi la wachezaji ambao hawakupata hata asilimia 50 ya playing time.

Mlianza kwa Mohamed Outtara.
Tuliwaonya kuwa mchezaji bora huwezi kumpata kwenye timu kubwa isipokuwa ni star player ambaye umevunja benki kwa ajili yake. Timu yenye malengo makubwa kama Al Hilal sa Sudan isingeweza kumwachia mchezaji Outtara aje kwenu kama angekuwa dhahabu kwenye first 11 yao. Waliamua kuwapa kwakuwa hakuweza kufikia matarajio ya klabu yao.

Vivo hivyo imetokea kwa huyu SAWADOGO.

Timu kubwa kama Diffa El Jadid isingeweza kuwaachieni star player kwa USD 150K. Ni wazi kuwa Sawadogo alikuwa mchezaji msindikizaji kwenye kikosi chao kama alivyokuwa Outtara kwenye timu ya Al Hilal.

Mtani wangu ukafanywa mtaji kwa mara nyingine tena ukaliwa pesa zako. Sasa ni kheri ungepeleka hilo dau Power Dynamo FC mkashindane na jitihada za Bwana Hersi huko. Au mliogopa?

Kwa historia ya nyuma ya Sawa dogo wala hairidhishi.
Ismael Sawadogo:
RC Kadiogo ( Burkina Faso )
2017/18: Al Mabarra ( Lebanon )
2017/18: Salitas ( Burkina Faso )
2018/19 USO ( Burkina Faso )
2019/20: Al Arrabi ( Kuwait )
2019/20: AS Douanes ( Burkina Faso )
2020/21: ENPPI ( Misri )
2021/22: Diffa el Jadida ( Morocco )
Sawa kaja: Simba


Mchezaji gani bora anacheza msimu mmoja alafu anasepeshwa kwingine? Mtani ninakuonea huruma sana kwa kushindwa kufanya sajili za kushindana na w Hersi.

Sasa nasikia mmewapa mkono wa kwaheri Okwa na Akpani. Najua ndio wamesepa mazima maana hamjawahi mrudisha mchezaji mliyempeleka kwa mkopo.

Mtani JIFUNZE MEMA KWA PACHA WAKO. Majivuni yatakumaliza.
 
Msituvuruge fanyeni yenu. Kati yenu na sisi nani mwenye mafanikio zaidi mashidano ya kimataifa msimu huu? Kwa nini tupokee ushauri kutoka kwenu wakati nyie mpo shirikisho huko kwa losers?

Huyu kafanya kazi TANESCO miaka 6 na piq Outtara si mchezaji mbovu. Ukumbuki alikuwa achukue namba ya Onyango hadi Onyango akatishia kuondoka?

Mnataka tugombee wachezaji na nyie ili mjione mko level moja na sisi?
 
tunajuwa mnapenda vibovu hatahuyo bora ya kanute kazi kwenu kesho mnamtangaza makoso
 
Temesajili garasa garasa kweli, umuhimu wa Mo unategemea Simba kivurunda ndicho tutalivuna
 
Ngoja nikudokezee kitu kwa jinsi klabu ya simba ilivyotengeneza jina na kupata mafanikio ya hapa na pale Afrika usitegemee ikanunua wachezaji kwa bei chee hata kama mchezaji profioe ni ndogo lazima watatangaza dau kubwa ujue kwanini?

Simba ni klabu kubwa huwezi fananisha sajili za utopolo na za simba daima haiwezekani
Huyo Musondo mnaejisifu mmepata ana goli 21 kwa misimu 5 ni kambole mpya hapo utopoloni hongereni sana kazi itakuwa kulisha mapumba na maji kwa msukule wenu mpya
 
Mpaka siku mnatoa mwiko nadhani akili zitawajia,haya wewe mbelemwikonyumamwiko hebu fanya hesabu ya magarasa mliosajili kuanzia 2019~2023 ALAFU UJE UTOE UJINGA WAKO,hivi kwa kipi ambacho unaweza kuutangazia umma kuwa utopolo ni bora kwa lipi hasa?timu bora zote zipo klabu bingwa AFRIKA
 
Nilipoona hayo maneno "ngoja nikueleze" nikajua una madini yakueleza kumbe ni ujinga wakitanzania huu!!, Duniani kote timu kubwa haizishindwi kuchukua top players wa ligi yoyote..... Ukubwa huonesha na facilities, usajiri na makombe tu nje ya hapo ni ubumbu wenu unasumbua. Timu kubwa imeshindwa kuvunja mkataba wa 400m? 😅
 
Subirini aanze kucheza ndio mpige hizi kelele zenu, tatizo lenu mna haraka sana[emoji850][emoji850][emoji850]
Kama tulivyo msubiri Outtara, Akpaan na Okwa si ndio?
 
Mchezaji mkubwa kutoka timu kubwa hauzwi kwa faranga za karanga.
 
Unawza ukavunja mkataba wa milioni 400 na bado ukalamba garasa
Punguan waheed
 
Unawza ukavunja mkataba wa milioni 400 na bado ukalamba garasa
Punguan waheed
Unavunjanja mkataba kwa mchezaji lonyalonya??, Unapoambiwa mchezaji kavunjiwa mkataba ujuwe yupo vizuri....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…