Simba SC wanapaswa kutafuta mwarobaini wa kuondoa sare kwenye mechi za kimataifa

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Natoa kongolee kwa wachezaji wa Simba sc kwa uwezo mdogo waliouonesha.

Lakini nitakua mtu wa mwisho kuamini kuamini kuwa Simba sc itafika robo kwenye michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE.

japo ni ukweli mchungu lakini watu wa mpira wataelewa nini namaanisha hii sare ya tatu Sasa kwa Simba SC, toka iingie kwenye michuano ya kimataifa imekua ngumu sana kupata matokeo.

Kocha wa Power dynamoo alisema "Simba sc ijiangalie kwa mpira wanavyocheza katika michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE"

Alizungumza kiufundi, wenye akili kubwa kama NALIA NGWENA tulimuelewa Nini ana maanisha.

Ikumbukwe mpaka Sasa Simba sc imeruhusu magoli 5 katika michuano ya kimataifa na ime droo/sare mechi tatu katika michuano hii ya kimataifa.

Kama litafumbiwa macho hili tatizo Basi Mashabiki wa Simba sc wajiandae kisaikolojia na sitegemei kuona simba sc ikifika robo kwa mwendo Sare na kuruhusu magoli katika kila mechi.
 
Acha twone
 
Wenye akili nyingi tumeelewa kuwa makolo makundi hawatoboi
 
Unaonaje ukawafundishe Simba?
 

Unateseka ukiwa wapi mkuu? Simba ipo 8 Bora africa kwa Sasa
 
Tangu jana mpaka leo huu ni uzi wako karibia wa 20 kuhusu Simba, tuweke utani pembeni hivi hunaga mambo mengine ya kimaisha tofauti na simba ?
Anaishi kwa dadake huyo,ipo siku shemeji yake atajifanya kalewa,shauri yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…