prince john john
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 2,184
- 3,369
1. Sina cha kuwalaumu Simba katika mazingira yale kwenda kwenye hatua ya upigaji wa mikwaju ya penati sio kazi ndogo. Well done Simba. Wapewe maua yao
2. Simba inahitaji marekebisho ya kiusajili. Wanapokwenda kusajili kwa Msimu Ujao waache kutafuta Yanga inataka kumsajili nani wamuaharibie bali wasikilize Matakwa ya Kocha anataka nini. Kwa dakika 90 Simba imeogopa kabisa kufanga Sub maana kwenye bench kulikuwa hakuna mchezaji mwenye quality ya waliokuwa ndani. Kwa timu kubwa kama Simba ni kosa kubwa kutokuwa na wachezaji wanaobaki nje wanaoweza kuamua kuubadilisha mchezo na kuumaliza kabisa.
3. Golikipa wa Simba Salum sio mbaya ila anakosa uzoefu. Penalt Zote kafungwa eneo Moja la upande wake wa Kulia. Naamini kwa Golikipa kama Manula kwa Uzoefu wake asingekosa hapo mbili. All in all hatuwezi mlaumu ni game kubwa sana kwake. Wapewe maua yao
4. Kwetu sisi Watanzania tunafundishwa namna ya kushangilia tuwapo uwanjani. Wenzetu wakiingia uwanjani wanaenda kufanya kazi sio kutongozana. Tukifikia hapo kwa mkapa mtu kula tatu itakuwa sio ajabu.
5. Africa inakumbushwa kuwa kuna taifa linakua kisoka ambalo ni Tanzania. Wengi walitarajia Simba angepigwa zaidi ya tano ila wamewazuia Whydad hadi Mashabiki wakapona ukichaa wao. Simba wapewe maua yao
6. Kwa Tunaofuatilia Soka tunaona Simba inasogea. Kabla ya Simba kufika Robo Fainal ilikuwa ikitolewa kwenye mtoano baadaye wakaweka malengo lazima tuende makundi, wakafanikiwa kwa kupambana baadaye lazima twende Robo na wamefika si mara Moja sasa naiona kiu na Tamaa yao kufika Nusu. Maendelee ni Process naamini hii kiu ya Nusu fainal watafika siku sio nyingi.
7. Bado marefa wetu wanaongozwa na pressure ya Timu mwenyeji. Isingekuwa Refa kuwavuruga Simba Kisaikolojia kipindi cha Kwanza pale Casablanca mabomu yangepigwa usiku huu. Refa kaonyesha udhaifu mkubwa sana wa kutoimudu Game.
8. Milioni 30 za Mama zinatosha kufanya kikao cha Tathimini pale Msimbazi kuhusu hatua waliyofikia.... Wapewe maua yao
9. Kocha mnaye, msimfukuze hata akikosa vikombe vyote kwa kikosi hiki cha Simba Kocha anajitutumua haswa kupata matokeo. Apewe maua yake
10. Tuwape maua yao wametoka ila wametoka kiume….Sina cha kuwadai.