Simba SC wasitegemee kumpata Tena Jonas Mkude endapo atatambulishwa Mwananchi day Kama tetesi za Mkude kwenda Yanga zinavyoimbwa

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Nilimsikia Msemaji wa Simba sc Ahmedy Ally akijinadi kwa madaha akiwadanganya mashabiki kuwa Simba Sc itamuaga Jonas Mkude na kustaafisha jezi yake.

Hiyo ni kwa mbumbumbu tu wanaweza wakaunga mkono hoja ya Ahmedy Ally lakini kwa welevu Kama NALIA NGWENA hawawezi kukubaliana na hoja nyepesi hiyo iliyotamkwa na mtu asiyejua utamaduni wa Simba Sc na Yanga Sc.

Ni ngumu sana ikitokea mchezaji katambulishwa Yanga Sc/ Simba sc kurudi Tena upande wa pili ili afanyiwe sherehe ya kuagwa ni ngumu sana Tena sana na hicho kitu hakitotokea kabisa katika huu utamaduni wa timu za kariakoo.

Simba sc hamkujiandaa kumuaga Mkude Ila wazo la kumuaga lilikuja baada ya mashabiki kupiga makelele kutokana na muda aliokaa na makubwa aliyoyafanya Simba sc.

Endapo tetesi zitakua ni za kweli Mkude kwenda Yanga Sc Basi Simba sc msitegemee kumpata Mkude kwa niaba ya kumuaga Kama mnavyojinasibu.
 
Nilimsikia Msemaji wa Simba sc Ahmedy Ally akijinadi kwa madaha akiwadanganya mashabiki kuwa Simba Sc itamuaga Jonas Mkude na kustaafisha jezi yake....
Tunajaribu kuwafundisha ustaarabu wa mpira ila bado mna ushamba mwingi
 
Kumuaga Mkude sio tukio la umuhimu sana kwa Simba,ukizingatia alikua kinara wa kuvunja nidhamu.
Simba ina wachezaji wengi wenye nidhamu wa kuwaaga kwa heshma.
Kwani Nani kadraft na kulipa airtime Kama wiki nzima?

Lina umuhimu ndiyo maana viongozi wa Simba wakalizungumzia.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mkimuacha akaenda kuagwa mtapungukiwa nini?
 
Yaani we jamaa una kaujuaji kakijinga sana. Yaani mkude asiagwe kwa sababu ni mchezaji wa yanga? Yanga ni kama singida fountain au kmc au prisons kwa hiyo ataagwa tu.
 
Mkude kasajiliwa yanga kwa kandarasi ya mwaka mmoja. Hakuna tetesi hapo
 
Unamjua gharib wewe? Kama ameweza kuingiza jezi nyeusi kuwa home kit badala ya kijani atashindwa vp kumruhusu mkude kuagwa simba? Kumbuka gharib ni ssc damu
 
Huyu mkude si mlisema mzee imekuaje leo kawa under 20 mnamtaka hahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…