Yameibuka madai kwamba Simba SC imefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na kocha wake msaidizi Selemani Matola.
Madai hayo yamechochewa na barua inayodaiwa kuandaliwa na Simba kusambaa mitandaoni.
- Tunachokijua
- Madai ya kuvunjwa kwa mkataba wa Kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola zimeanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, leo Oktoba 28, 2022.
Mathalani, mtumiaji mmoja wa mtandao wa X ameweka ujumbe ukiambatana na picha ya tangazo la kufutwa kazi kwa kocha Matola.
JamiiForums imefanya mawasiliano na Meneja wa Kitengo Cha habari cha Simba (Ahmed Ally) ambaye amesema kuwa barua hiyo ni feki na wameamua kuipuuza.
Ahmed Ally ameongeza kuwa kama taarifa hiyo Ingekuwa na ukweli basi ingepandishwa na kuwekwa wazi katika kurasa rasmi za klabu.
Selemani Matola aliwahi kuwa mchezaji wa Simba aliyepata mafanikio makubwa. Baada ya kucheza Soka Afrika Kusini kisha kustaafu, alijiunga na timu yake za Zamani kama kocha wa timu za vijana na sasa anahudumu kama kocha wa timu za vijana za Simba.