Simba SC yaigaragaza Mbeya City goli 3-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar

Simba SC yaigaragaza Mbeya City goli 3-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Timu za Simba na Mbeya City tayari zimeshaingia uwanja wa Taifa tayari kwa mtanange. Baada ya jana Yanga kushurutishwa sare na walima alizeti, Simba inashika usukani kwa tofauti ya alama tano ilhali wakiwa na michezo sawa.

Fuatana nami nikujuze kinachojiri dimba la Taifa mechi kati ya kinara Simba Vs Mbeya City.
=======

Akiongea kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema anatarajia mchezo mzuri na atafurahi tofauti ikiwa zaidi ya alama 5 kuliko chini yake kwani itawafanya wawe salama zaidi.

Kocha wa Mbeya City kwa upande wake amesema presha iko kwa Simba kwa sababu wanatafuta ubingwa, amesema mchezaji akicheza kwa Moyo na bidii chochote kinaweza kutokea uwanjani.

======

00' Refa anapiga filimbi kuashiria mwanzo wa mchezo

02' Simba wanapata kona ya kwanza, wanapiga fupi lakini unakuwa mpira wa offside walipojaribu tena kuutumbukiza kati.

11' Ngaya anajaribu shuti la mbali lakini mlinda mlango anasimama imara langoni mwa Simba na kudaka kiulani.

14' Okwi anapoteza fursa adhimu kutia kimiani baada ya krosi safi kutoka kwa John Bocco

16' Okwiiiiii, Anapiga bao lake la 18 kwenye ligi baada ya mpira wa Bocco kuzuiwa na beki wa Mbeya City, anaubeba na kuumalizia kiulaini. Simba 1-0 Mbeya City.

19' Mkude anaachia shuti kali na kumbabatiza beki wa Mbeya city kutengeneza kona pacha ambayo haijazaa matunda.

32' Asante Kwasi anaiandikia Simba bao la pili, wachezaji Mbeya City walijaribu kucheza offside, Simba 2-1 Mbeya City.

33' Mbeya City wanarudisha bao moja kwa mpira wa kona na Nkobela kunganisha kwa mpira wa kichwa. Simba 2-1 Mbeya City.

34' Bocco anaiandikia Simba bao la tatu baada ya krosi safi kutoka kwa Kapombe, Simba 3-1 Mbeya City.

38' Mbeya city wanapata kona 3 za haraka haraka lakini zote zinashindikana kuzaa matunda.

45+1' Mpira umeenda mapumziko
 
Attachments

  • Simba.jpg
    Simba.jpg
    107 KB · Views: 72
sawa mkuu tunafatilia MTAnange humuhumu JF. cjutii kutumia jf
 
Timu za Simba na Mbeya City tayari zimeshaingia uwanja wa Taifa tayari kwa mtanange. Baada ya jana Yanga kushurutishwa sare na walima alizeti, Simba inashika usukani kwa tofauti ya alama tano ilhali wakiwa na michezo sawa.

Fuatana nami nikujuze kinachojiri dimba la Taifa mechi kati ya kinara Simba Vs Mbeya City.
=======

Akiongea kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema anatarajia mchezo mzuri na atafurahi tofauti ikiwa zaidi ya alama 5 kuliko chini yake kwani itawafanya wawe salama zaidi.

Kocha wa Mbeya City kwa upande wake amesema presha iko kwa Simba kwa sababu wanatafuta ubingwa, amesema mchezaji akicheza kwa Moyo na bidii chochote kinaweza kutokea uwanjani.
Weka kikosi cha munyama
 
Game ya leo ni ngumu kwetu Simba hesabu hazijakaa sawa hv.

Ngoja tuone hz mechi za ubingwa hakuna mtelemko ni kubana matako mwanzo mwisho.

SIMBA NGUVU MOJA
 
mama watoto wangu kwao Mbeya.
kaapa nisipo-support Mneya City leo nisahau unyumba hadi June.
sina jinsi, leo inabidi tu niwe Mbeya City...uzuri wenyewe adhabu hii ni ya dk 90 tu.
wakuu, ungekuwa wewe hata kama ni Simba damu ungekubali kweli?
looooh!!
 
Back
Top Bottom