Simba SC yaingia makubaliano rasmi ya udhamini na kampuni ya SportPesa kwa kipindi cha miaka 5

Cicadulina

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
977
Reaction score
2,370
Wekendu wa msimbazi leo wameingia mkataba na kampuni ya kubetisha ya SPORTPESA kwa
ajili ya udhamini katika ligi kuu bara kuanzia msimu ujao.

Simba imeingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya shilingi bilioni 4.9 Ni mkataba mkubwa kupita mikataba yote ambayo Simba wamewahi kuisaini.

Hongereni wanaSimba






 

Attachments

  • Untitled.jpg
    21.7 KB · Views: 54
Nilidhani utatuwekea pia matokeo hadi sasa kumbe unatuonesha nguo. Dah! Haya
 
Quality Group zamu inakuja kesho msikonde
 
Huyu tarimba si alikua gaming board?kabla ya hapo Yanga?haha leo anawadhamini Simba.
 
Kikubwa mafanikio tu..kama sport pesa walifanikiwa ulaya iweje washindwe hapa kwetu? Hongera wekundu wa msimbazi! Matarajio yetu sisi kama wapenzi na mashabiki wa Simba ni usajili wa maana wenye kuleta tija na hamasa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, club iwe na miradi endelevu ya kupata kipato nje ya udhamini, bila kusahau kumalizia uwanja pale bunju..Vivaaa Simbaaaaa...mwafulani ameugomea mkataba au hah hah
 
Safi ila watuwekee mkataba tujue tumefaidikaje na iyo spotpesa
 
Betting inalipa aisee ..sio kwa uwekezaji Huu.. Wanakaba kila kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…