Wakuu,
Nimeona mtandaoni kuwa simba imemfuta kazi kocha wake wa Makipa Dani Cadena alizotoa kwenye vyombo vya habari akidai kuingiliwa kwenye majukumu yake.
JamiiCheck tusaidieni kuihakiki maana sijaiona kwenye page rasmi za simba.
Nimeona mtandaoni kuwa simba imemfuta kazi kocha wake wa Makipa Dani Cadena alizotoa kwenye vyombo vya habari akidai kuingiliwa kwenye majukumu yake.
JamiiCheck tusaidieni kuihakiki maana sijaiona kwenye page rasmi za simba.
- Tunachokijua
- Tangu kumalizika kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Klabu ya simba imekuwa ikipitia wakati mgumu unaohusisha maneno mbalimbali kutoka kwa Wachezaji, viongozi, Mashabiki na Wanachama wake. Mashabiki wengi hawajaridhishwa na timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu jambo linalopelekea timu hiyo kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika badala ya Ligi ya Mabingwa kama ilivyokuwa miaka mitano nyuma.
Kuanzia Juni 8 kumekuwa na video (hii) inazunguka ikimuhusisha Kocha wa Makipa Simba akieleza changamoto mbalimbali za kiutawala na kimfumo za Klabu ya Simba. Suala hili limeendelea kuchochea moto na migogoro ndani ya Klabu ya simba.
Kufuatia sakata la Kocha huyo kuzungungumza na Mwanahabari kueleza changamoto za ndani ya Simba kumeibuka barua hiyo ikidai Mkurugenzi Mtendaji wa Simba akiiandika kufuta kazi kocha huyo.
Je, upi ukweli kuhusu barua hiyo?
JamiiCheck imepitia katika kurasa rasmi za mitandao ya Kijamii za Klabu ya simba pamoja na ukurasa rasmi wa Instagram wa Mtendaji Mkuu Imani Kajula lakini haujakutana na barua wala taarifa ya Kocha wa Makipa kufukuzwa kazi.
JamiiCheck imewatafuta viongozi wa Simba ambao hawajapatikana, lakini imempata mtu wa ndani ambaye hajataka jina lake liwekwe wazi, amesema:
Mikataba wa kocha umeisha mwisho wa msimu huu uliomalizika (2023/24) klabu haikuwa na mpango wa kumuongezea Mkataba kwa kuwa linakuja benchi jipya la ufundi. Amezungumza hayo akijua Simba hawana mpango naye na siyo kwamba amefukuzwa.
Hivyo, kwa kauli hiyo ya Mfanyakazi wa Simba ni ishara kuwa barua ya kumfukuza kazi Kocha Cardena haina ukweli.