SI KWELI Simba SC yamfuta kazi Dani Cadena kwa madai ya kuingiliwa katika majukumu ndani ya klabu

SI KWELI Simba SC yamfuta kazi Dani Cadena kwa madai ya kuingiliwa katika majukumu ndani ya klabu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,

Nimeona mtandaoni kuwa simba imemfuta kazi kocha wake wa Makipa Dani Cadena alizotoa kwenye vyombo vya habari akidai kuingiliwa kwenye majukumu yake.

JamiiCheck tusaidieni kuihakiki maana sijaiona kwenye page rasmi za simba.

SImba fake.jpg
 
Tunachokijua
Tangu kumalizika kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Klabu ya simba imekuwa ikipitia wakati mgumu unaohusisha maneno mbalimbali kutoka kwa Wachezaji, viongozi, Mashabiki na Wanachama wake. Mashabiki wengi hawajaridhishwa na timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu jambo linalopelekea timu hiyo kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika badala ya Ligi ya Mabingwa kama ilivyokuwa miaka mitano nyuma.

Kuanzia Juni 8 kumekuwa na video (hii) inazunguka ikimuhusisha Kocha wa Makipa Simba akieleza changamoto mbalimbali za kiutawala na kimfumo za Klabu ya Simba. Suala hili limeendelea kuchochea moto na migogoro ndani ya Klabu ya simba.

Kufuatia sakata la Kocha huyo kuzungungumza na Mwanahabari kueleza changamoto za ndani ya Simba kumeibuka barua hiyo ikidai Mkurugenzi Mtendaji wa Simba akiiandika kufuta kazi kocha huyo.

Je, upi ukweli kuhusu barua hiyo?
JamiiCheck imepitia katika kurasa rasmi za mitandao ya Kijamii za Klabu ya simba pamoja na ukurasa rasmi wa Instagram wa Mtendaji Mkuu Imani Kajula lakini haujakutana na barua wala taarifa ya Kocha wa Makipa kufukuzwa kazi.

JamiiCheck imewatafuta viongozi wa Simba ambao hawajapatikana, lakini imempata mtu wa ndani ambaye hajataka jina lake liwekwe wazi, amesema:

Mikataba wa kocha umeisha mwisho wa msimu huu uliomalizika (2023/24) klabu haikuwa na mpango wa kumuongezea Mkataba kwa kuwa linakuja benchi jipya la ufundi. Amezungumza hayo akijua Simba hawana mpango naye na siyo kwamba amefukuzwa.

Hivyo, kwa kauli hiyo ya Mfanyakazi wa Simba ni ishara kuwa barua ya kumfukuza kazi Kocha Cardena haina ukweli.
Hii ililetwa kuanzia juzi tukasema ni fake news

Cadena alishamaliza mkataba na alishaondoka Simba, unamfukuzaje kazi mtu ambae sio muajiriwa wako tena
 
Barua ina makosa mengi sana ya kisarufi! CEO mzima wa klabu kama Simba hawezi kupitisha hii barua! Labda awe chizi!
 
Wakuu,

Nimeona mtandaoni kuwa simba imemfuta kazi kocha wake wa Makipa Dani Cadena alizotoa kwenye vyombo vya habari akidai kuingiliwa kwenye majukumu yake.

JamiiCheck tusaidieni kuihakiki maana sijaiona kwenye page rasmi za simba.

View attachment 3012861
Za kweli hizi au uchochezi tu mnataka kumchafua huyu jamaa?
 
Wakuu,

Nimeona mtandaoni kuwa simba imemfuta kazi kocha wake wa Makipa Dani Cadena alizotoa kwenye vyombo vya habari akidai kuingiliwa kwenye majukumu yake.

JamiiCheck tusaidieni kuihakiki maana sijaiona kwenye page rasmi za simba.

View attachment 3012861
HAHAHAH Kasema ukweli tuu kashakua sio mpenda mafanikio!!soka letu kivyetuvyetu!!
 
Back
Top Bottom