Simba SC yarejea Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wake na Yanga

Simba SC yarejea Dar kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wake na Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
SIMBA1.jpg

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar

Kikosi cha Simba kimeondoka Visiwani Zanzibar leo asubuhi kwa ndege kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Uhuru.

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema akili yao yote ni kuifunga Yanga kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwataka Mashabiki wa Simba waende uwanjani kwa wingi kuishangilia timu yao.

"Kambi ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana naamini tumefikia malengo yetu, hapa tunaondoka na leo jioni Dar tutafanya mazoezi ya mwisho, nawaomba Mashabiki wa Simba wazidi kuishangilia timu yao,” Manara ameuambia mtandao huu wakati waondoka hapa Zanzibar kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Simba walikuwa kambini mjini hapa tangu Jumatatu ya Oktoba 23 na leo Ijumaa Oktoba 27 wamerejea nyumbani Dar es salam kuwavaa Yanga.

Chanzo: Shaffih Dauda
 
Back
Top Bottom