Simba SC yatangaza rasmi kumuuza kiungo wake Left Footer Magician Rally Bwalya

Simba SC yatangaza rasmi kumuuza kiungo wake Left Footer Magician Rally Bwalya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya Simba yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi Jijini Dar es salaam leo Juni 17 2022, imetangaza rasmi kumuuza kiungo wake Left Footer Magician, Rally Bwalya raia wa Zambia.

"Tumefikia makubaliano ya kumuuza mchezaji wetu Rally Bwalya". Imeeleza kwa ufupi taarifa hiyo kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kufuatia taarifa hiyo, mchezo wa Jumapili Simba SC dhidi ya KMC utatumika kumuuaga Kiungo huyo Left Footer Magician Rally Bwalya, mtaalamu wa pasi za kudondosha nyuma ya mabeki.

klabu ya Simba haijaweka wazi Ada na klabu yake mpya ambayo anakwenda kuitumikia, ilielezwa ni kutokana na matakwa ya kimkataba, hata hivyo Bwalya amekuwa akiwindwa na Amazulu FC ya Afrika Kusini.
 
Unauzaje mchezaji aliyemaliza mkataba?. Ifike mahali Simba waache kutudanganya mashabiki. Si ajabu wakatuambia hata Musa Phil wamemnunua wakati inafahamika alikuwa mchezaji huru.
Huyo mkataba wake umebakia siku kadhaa nadhani unakwisha tarehe 14.07.2022, sasa nashindwa kuelewa etu ameuzwa!

Vilabu vyetu vinakuwa na uswahili sana na haswa Simba
 
Wapuuzi sana. Uongo mwingi hata pasipotakiwa. Kila kitu wanaleta ujanjaujanja. Bwalya ameondoka bure.
Simba baada ya kuangukia pua msimu huu wamebaki wanatafuta jinsi ya kutuhadaa mashabiki kwa ulaghai usio na tija.

Acha kukutupuka, Bwalya alisaini miaka mitatu (3) kipindi ananunuliwa na ametumikia miaka miwili ulikua bado mwaka mmoja.
 
Hawajasema Ada ya uhamisho ilielezwa ni kutokana na matakwa ya kimkataba baina ya klabu kwa pande zote mbili.
Hela zenyewe chache hazina haja ya kutajwa.

Imagine wenzetu wanauza mchezaji 1 kwa Bilioni 98 ambapo klabu zetu hicho kiasi hakiwezi kufikiwa kwa msimu mzima kwenye mapato
 
Hongereni Simba kwa kumuuuza Bwalya. Bwalya alikuwa na kipaji kikubwa sana lakini mchango wake kwenye timu ulikuwa unashuka siku hadi siku tofauti kabisa na alivyofika Simba kwa mara ya kwanza. Ni wakati sasa wa kuijaza nafasi yake kwa kutafuta mchezaji wa kiungo mwenye kasi ya kuichangamsha timu pale katikati pamoja na uwezo wa kupora mipira/kukaba kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom