Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Vigogo wa Tanzania, Simba SC wamethibitisha kumsajili Elie Mpanzu Kibisawala kwa mkataba wa miaka miwili akitokea As Vita Club.
Mpanzu anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya Premier League mapema mwakani. Hata hivyo, winga huyo huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha Simba kinachoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa ajili ya mechi zijazo za hatua ya makundi.
Mpanzu anakwenda kujiunga na washambuliaji wengine wa timu hiyo ambao; Valentino Mashaka, Kibu Denis, Lionel Ateba na Steven Mukwala.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba Mpanzu atajiunga na kikosi hivi karibuni.