Simba sio timu tajiri

Utajiri wa Team kama Simba hauko kwenye kitu kingine chochote zaidi ya jina, wahasibu wanaita Goodwill huwezi kuamini Goodwill kimahesabu inawekwa kwenye Fixed Asset
Benki kama Nmb, Crdb au Nbc wakati zinauzwa wawekezaji waliozinunua walinunuwa na majina yake. Nimetoa hiyo mifano ili nionyeshe nguvu ya jina katika biashara hususan ya mpira
Nyinyi nyote ni mashahidi jinsi Moo alivyoinunua African Llions lakini ikashindwa kukidhi mahitaji ya kibiashara akaipandisha daraja Singida United lakini haikufua dafu na hivyo hivyo ndivyo ilivyo tokea kwa Azam
Mchezaji wa kawaida anaona bora akaichezee Simba au Yanga kuliko Azam hata kama kuna tofauti ya mshahara wa 2m simply became kuna benefits nyingi anazipata akiwa mtaani akijulikana kama ni mchezaji wa Simba au Yanga
Kwa kifupi huo ndio utajiri walio nao Simba na Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…