Simba Sport Club: Taarifa kwa umma

Simba Sport Club: Taarifa kwa umma

SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
2-10-2016

TAARIFA KWA UMMA

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba imesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wetu,cha kuvunja sehemu ya viti vya Uwanja wa Taifa.kitendo kilichotokea jana kwenye mchezo wetu wa Ligi kuu dhidi ya Timu ya Yanga.

Tungependa kuomba radhi kwa kadhia hii na klabu imekubali kulipia gharama za uharibifu huu.
Klabu itazungumza na wamiliki wa Uwanja huu kuona inalipaje gharama hizo.
Ni mategemeo yeti kuona jambo hili halitajikoze tena.

Lakini mbali na hayo klabu kesho Jumatatu itawasilisha malalamiko rasmi juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi wa mchezo wa jana,hususan Mwamuzi wa kati Martin Sanya.

Sisi tunaamini vitendo viovu vilivyofanywa na washabiki wetu vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita kiasi uliosababishwa na waamuzi hao.

Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo alitumia kulikubali goli la 'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe na kulikataa goli halali la mshambuliaji wetu Ibrahim Ajibu.

Pia tumeshangazwa na kitendo cha kumpa kadi nyekundu nahodha wetu Jonas Mkude.ilhali kama nahodha alimfata kwenda kumlalamikia kitendo chake cha kukubali goli la 'hovyo 'la Tambwe.
Sote tumeona Sanya alijikwaa wakati anarudi nyuma na kuanguka,kisha kuanguka na kutoa kadi nyekundu kwa Mkude.

Kimsingi huyu mwamuzi ana historia ovu ya kuwabeba Yanga.
Hakuna asiyesahau msimu uliopita kwenye kombe la Shirikisho,Yanga walipocheza na Coastal Union kule Mkwakwani Tanga.nini kilitokea!

Tunajua safari hii Tff na bodi ya Ligi zitatoa adhabu kali kwa waamuzi hawa ili iwe fundisho kwa maamuzi ya hovyo ya aina hii.

Pia klabu italalamika kitendo cha vyumba vyetu vya kubadilishia nguo(dressing room)kupuliziwa dawa zilizokuwa na nia ya kuwaathiri wachezaji wetu kabla ya mechi kuanza.

Tutaziomba mamlaka zifanye uchunguzi wa kina kubaini kitendo hiki kisicho cha kiungwana kinachosadikiwa kufanywa na wapinzani wetu.
Tunajua dhamira yao ni kuwafanya wachezaji wetu wachoke,lakini timu yetu ya Matabibu ilichukua hatua sahihi za kuwafanya wachezaji wetu waweze kumaliza dakika Tisini za mchezo kwa uwezo na weledi mkubwa.

Na mwisho klabu itoe malalamiko yake kwa Waziri wa mambo ya nchi,Mh Mwigulu Nchemba.

Waziri huyu bila shaka amesahau majukumu yake yake ya kazi na kugeuka kiongozi wa klabu ya Yanga.

Tunajua ni haki yake kuwa na mapenzi kwa klabu aliyoichagua.lakini vitendo vyake anavyovifanya vinaacha maswali mengi kuliko majibu.ukizingatia nafasi yake kama Waziri mwenye dhamana ya kuongoza Wizara nyeti.

Itakumbukwa majuzi waziri huyu alifanya ziara Mkoani Morogoro kuzungumza na vikosi anavyoviongoza.
Na inajulikana pia Refarii wa mchezo wa jana Martin Sanya ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro

Sote tulishuhudia Jana Mwigulu alishangilia goli la hovyo la mwajiriwa wake Sanya.

Pia waziri huyu alitoa kauli tata kuwa angetamani siku moja klabu inayoshangilia wapinzani wa Yanga wakipigwa mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la Polisi.
Kauli hii aliitoa wakati wa sherehe za kukabidhi zawadi kwa timu zilizoshinda msimu uliopita zilizoandaliwa na wadhamini wa ligi.kampuni ya Vodacom.

Tunajiuliza yale mabomu ya jana pale Uwanja wa Taifa ndio utekelezaji wa maagizo ya boss Mwigulu?

Lakini pia matumizi ya rasilimali za umma yakiwemo magari ya serikali ktk shughuli za mara kwa mara za klabu ya Yanga napo kunaacha maswali mengi mno.

Wanasimba wanauliza kila Waziri anayeshabikia Simba akiwepo Waziri Mkuu akifanya vitendo hivi kutakuwa na utawala gani serikalini?

Imani yetu viongozi wakuu wa nchi watamuonya mh Mwigulu,vingenevyo atatengeneza chuki baina ya washabiki wa Simba dhidi ya serikali yao.
Mwigulu atambue klabu ya Simba ina mamilioni ya washabiki kama ilivyo klabu yake anayoishabikia.

Hatutarajii kuona 'mahaba'yake yasio na staha yanachochea jambo ovu kwa wanasimba na serikali yao wanayoiamini na kuipenda sana.

IMETOLEWA NA
KLABU YA SIMBA

SIMBA NGUVU MOJA
Simba wa serengeti
 
Simba wahuni tu lipeni gharama za uwanja wetu wa Taifa kisha mjenge wenu Bunju muwe mnang'oa viti vyenu wenyewe, Yanga ilifungwa 5-1 na red card mbili haikung'oa kiti hata kimoja

Ilifungwa 5-0 siyo 5-1 Si mngejidai kuwa mlichomoa kimoja.
Kwa kweli suala la kung,oa viti halipendezi,, zamani kule kwenye shamba LA Bibi watu walisimama kwenye mabomba had mwisho wa game.,
Leo watu wanaangalia mpira wamekaa raha mustarehe eti MTU anang,oa kiti ili sijui iweje,,
Tujivunie uwanja wetu tusiuharibu ni Aibu kwetu.
Tff nao watafute waamuzi wenye sifa waache masihara na hizi Big match.
 
Wakati tunaanza ligi nilisema.TFF msimu huu lazima wajirekebishe.Habari ya kuelekeza marefa kutazua maafa.Naona jana yamedhihirika, kiongozi wa soka hutakiwi kuonyesha upande wowote wa ushabiki wako.kuna siku watu tulijadili account ya mh.fulani kwamba ameandika "NAIPENDA YANGA".Nilijiuliza kama yeye ni baba wa wote,timu zingine zipendwe na nani?
 
Simba wahuni tu lipeni gharama za uwanja wetu wa Taifa kisha mjenge wenu Bunju muwe mnang'oa viti vyenu wenyewe, Yanga ilifungwa 5-1 na red card mbili haikung'oa kiti hata kimoja
Ilifungwa kihalali na refavalikuwa wenu mnajua hilo,mnajua mlizidiwa mchezo,nguvu za kung'oa mnazitoa wapi?
 
unajua watz tuna shida snki ukweli coz kuna uhusiano gani kati ya goli la Tambwe na viti?? hivi ni mara ya kwanza goli kufungwa tena kwa mkono katika ulimwengu wa soka??hivi tunawezaje kumlaumu refa kwa kila jambo kwani yeye si binadamu??mfano golila Ajibu aliyesema sio goli ni mshika kibendera wa upande ule kuwaaliotea kitu ambacho kinasadikika haikuwa ameotea sasa kwanini tumlaumu sanya??Afu goli la Tambwe refa alikuwa karibu lkn kwa alivyogeuka Tambwe ni sekunde ilikuwa so kuona moja kwa moja kama aliunawa ule mpira ilikuwa ngumu so tusilaumu sana tukashindwa kufanya mambo ya maendeleo.
Isitoshe jiulizeni ile ilikuwa ni.mpira kufuata mkono au mkono ulifuata mpira???
so tuache kulalamika lalamika tujipange kisoka matokeo hayabadiliki tutabaki tunalalamika tuuu hata maradona alifunga kwa mkono na kombe la dunia kabeba.
Acha siasa huu ni mpira wa miguu una sheria zake 17!Unashindwaje kuona dhulma inavyoweza kuamsha hasira?Acha mahaba tizama ukweli
 
Ilifungwa kihalali na refavalikuwa wenu mnajua hilo,mnajua mlizidiwa mchezo,nguvu za kung'oa mnazitoa wapi?
Vipi kuhusu yule mama refarii?nyie kulalamika hamjaanza leo,mnacholazimisha ni kutaka kushinda wakati uwezo haupo,endeleeni kulalamika na kung'oa viti.
 
Pumbufu zenu kweli. Kwa hiyo nyie mnahalalisha kuzuia kosa kwa kutenda kosa?
Kama unachoandika hapa!!Inzi ni inzi tu hata akiruka juu hawezi kuwa ndege.Naona kwa sasa unajidanganya kuwa wewe ni ndege ila sisi tunaona inzi tuu!
 
Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba imesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wetu,cha kuvunja sehemu ya viti vya Uwanja wa Taifa.kitendo kilichotokea jana kwenye mchezo wetu wa Ligi kuu dhidi ya Timu ya Yanga.

Tungependa kuomba radhi kwa kadhia hii na klabu imekubali kulipia gharama za uharibifu huu.
Klabu itazungumza na wamiliki wa Uwanja huu kuona inalipaje gharama hizo.
Ni mategemeo yeti kuona jambo hili halitajikoze tena.

Lakini mbali na hayo klabu kesho Jumatatu itawasilisha malalamiko rasmi juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi wa mchezo wa jana,hususan Mwamuzi wa kati Martin Sanya.

Sisi tunaamini vitendo viovu vilivyofanywa na washabiki wetu vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita kiasi uliosababishwa na waamuzi hao.

Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo alitumia kulikubali goli la 'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe na kulikataa goli halali la mshambuliaji wetu Ibrahim Ajibu.

Pia tumeshangazwa na kitendo cha kumpa kadi nyekundu nahodha wetu Jonas Mkude.ilhali kama nahodha alimfata kwenda kumlalamikia kitendo chake cha kukubali goli la 'hovyo 'la Tambwe.
Sote tumeona Sanya alijikwaa wakati anarudi nyuma na kuanguka,kisha kuanguka na kutoa kadi nyekundu kwa Mkude.

Tunajua safari hii Tff na bodi ya Ligi zitatoa adhabu kali kwa waamuzi hawa ili iwe fundisho kwa maamuzi ya hovyo ya aina hii.

Pia klabu italalamika kitendo cha vyumba vyetu vya kubadilishia nguo(dressing room)kupuliziwa dawa zilizokuwa na nia ya kuwaathiri wachezaji wetu kabla ya mechi kuanza.

Tutaziomba mamlaka zifanye uchunguzi wa kina kubaini kitendo hiki kisicho cha kiungwana kinachosadikiwa kufanywa na wapinzani wetu.
Tunajua dhamira yao ni kuwafanya wachezaji wetu wachoke,lakini timu yetu ya Matabibu ilichukua hatua sahihi za kuwafanya wachezaji wetu waweze kumaliza dakika Tisini za mchezo kwa uwezo na weledi mkubwa.

Na mwisho klabu itoe malalamiko yake kwa Waziri wa mambo ya nchi,Mh Mwigulu Nchemba.

Waziri huyu bila shaka amesahau majukumu yake yake ya kazi na kugeuka kiongozi wa klabu ya Yanga.

Tunajua ni haki yake kuwa na mapenzi kwa klabu aliyoichagua lakini vitendo vyake anavyovifanya vinaacha maswali mengi kuliko majibu ukizingatia nafasi yake kama Waziri mwenye dhamana ya kuongoza Wizara nyeti.

Itakumbukwa majuzi waziri huyu alifanya ziara Mkoani Morogoro kuzungumza na vikosi anavyoviongoza.
Na inajulikana pia Refarii wa mchezo wa jana Martin Sanya ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro

Sote tulishuhudia Jana Mwigulu alishangilia goli la hovyo la mwajiriwa wake Sanya.

Pia waziri huyu alitoa kauli tata kuwa angetamani siku moja klabu inayoshangilia wapinzani wa Yanga wakipigwa mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la Polisi.
Kauli hii aliitoa wakati wa sherehe za kukabidhi zawadi kwa timu zilizoshinda msimu uliopita zilizoandaliwa na wadhamini wa ligi.kampuni ya Vodacom.

Tunajiuliza yale mabomu ya jana pale Uwanja wa Taifa ndio utekelezaji wa maagizo ya boss Mwigulu?

Lakini pia matumizi ya rasilimali za umma yakiwemo magari ya serikali ktk shughuli za mara kwa mara za klabu ya Yanga napo kunaacha maswali mengi mno.

Wanasimba wanauliza kila Waziri anayeshabikia Simba akiwepo Waziri Mkuu akifanya vitendo hivi kutakuwa na utawala gani serikalini?

Imani yetu viongozi wakuu wa nchi watamuonya mh Mwigulu,vingenevyo atatengeneza chuki baina ya washabiki wa Simba dhidi ya serikali yao.
Mwigulu atambue klabu ya Simba ina mamilioni ya washabiki kama ilivyo klabu yake anayoishabikia.

Hatutarajii kuona 'mahaba'yake yasio na staha yanachochea jambo ovu kwa wanasimba na serikali yao wanayoiamini na kuipenda sana.

IMETOLEWA NA
KLABU YA SIMBA

SIMBA NGUVU MOJA
 
Simba wahuni tu lipeni gharama za uwanja wetu wa Taifa kisha mjenge wenu Bunju muwe mnang'oa viti vyenu wenyewe, Yanga ilifungwa 5-1 na red card mbili haikung'oa kiti hata kimoja
We ni mtu mzima weka mahaba pembeni na useme ukweli katk zile goli tano kuna goli la mkono
 
Zaidi ya milioni 300 zinahitajika kukarabati viti vilivyoharibiwa jana bila kujumlisha gharama za kutengeneza mageti yaliyovunjwa. Kila kiti kimoja kina gharimu Tshs 200,000
 
1475422302185.jpg
 
Mwigluu aache kiherehere nae ni kwl kbisa huwez kutumia rasilimali za gvt hasa hii inayobana matumizi kwa aajili ya mambo binafs maana huko yanga hata uongozi hana
 
Upuuzi mtupu, sidhani kama umma watakubaliana na hio taarifa.
 
Back
Top Bottom