Simba sport club wazindua tovuti yake

Simba sport club wazindua tovuti yake

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
203
Reaction score
83
AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba


Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza mawasiliano na wadau wake mbalimbali hususani; wanachama, wapenzi, vyombo vya habari na wadau wengine muhimu.

Akizungumza wakati wauzinduzi huo Rais wa Simba Evans Aveva alisema ''Katika dunia na zama za utandawazi tovuti ndio na mitandao ya jamii ndio njia kuu ya mawasiliano. Sisi tuliliona hili na leo hii nafurahi kuwa Simba Sports Club itazindua rasmi tovuti yake ambayo itakuwa jukwaa kuu la mawasiliano na utoaji wa taarifa zake za club ya Simba.

Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu tovuti yetu''.

AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ''Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia itatumika kwa ajili ya uuzaji wa vifaa vya Simba, Bidhaa mbalimbali mpya na muhimu zaidi kuwaunganisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kutumia mitandao ya jamii iliyo rasmi ya Simba Sports Club''.

Mkutano huo wa wandishi wa habari ulitumika kutaarifu Wanachama, Wapenzina Vyombo vya habari juu ya kocha mpya wa Simba. Alizungumza wakati wakumtambulisha kocha mpya wa Simba, Rais Aveva alisema ''Baada ya kupitia vyeti na maombi ya makocha mbalimbali, Napenda kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye mkataba wa kuifundisha na kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza. Ni kocha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30, akiwa amefanya kazi Nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Scotland, Vietnam na AfrikayaKusini''.

Aliendelea kusema ''Tunaamini ujuzi na uzoefu wake wa ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu utakuwa chachu ya kuifanya Simba ifanye vizuri''

 
mmmmm!! hii pira ya bongo ni shida sana!! hapo watawaaminisha mashabiki wao kuwa timu yao itatisha kwa kuchukua vikombe!!! kwabi ile tv yao iliishia wapi jamani?? uzuri wa website muwe na habari/products, sasa hapa nadhani habari kubwa zitakuwa ni fujo tu, na kesi za mikataba tu. wana habari gani mpya za ku i update? mambo mengi yaanaanzishwa kwa kukurupuka tu, ule mradi walioingia na bank ya posta, uko wapi?? ohh mala itakuwa mwisho wa kuomba omba yako wapi?? mpira wa nchi hii hadi hao wazee wa MUJINI, watakapouachia. kitu ambacho si rahisi, muulize MAICO MWAMBURA.
 
Hiyo website wanayoitangaza sana mbona sijaona anwani yake popote pale.
 
Hivi dunia ya sasa timu kama simba ilikuwa haina tovuti,hii ni aibu,!
 
Back
Top Bottom