Simba, Sportpesa hawakukutana barabarani


Swali zuri sana atueleze Simba inanyonywa vipi na Mo,
Huyu Bw.Mdogo ni Kiongozi wa Ndani ya Yanga na amekuwa akipitisha bakuri na Michango Haramu ya kuwahonga akina Kambuzi. Mpuuuzeni kama Watopolo wengine. Mbaya zaidi wengine tunamjua majina na mpaka na anapoishi. Leo tu hapa jukwaa la Michezo anazo nyuzi 3 zinazoishambulia Simba na MO kwa ujumla. Tunakuonya wewe Bw.Mdogo habari za Simba waachie wenye timu yao utakuja kutoka jasho la MENO!
 
Umeandika hoja yenye mashiko sana mtoa mada. Ila ni jambo la kushangaza mashabiki wa timu husika wanakimbilia tu kukukejeli na kukutupia kila aina ya maneno ya karaha!

Nakumbuka sana enzi zile timu zetu hizi mbili zilipokuwa mahututi huku Gor Mahia ya Kenya ikifaidi matunda ya hawa jamaa Sportpesa, kabla ya hao Sportpesa kuingia Bongo na kutoa udhamini ambao umezisaidia sana hizi klabu zetu mbili (Yanga na Simba)

Kimsingi Mo anatakiwa kuwa muwazi! Kama anaona Sportpesa wanatoa dau dogo, aahidi mbele ya Bodi ya Timu angetoa kiasi gani kama mdhamimi mkuu badala ya hao Sportpesa! Tofauti na hapo, ataonekana ana majungu na hana nia nzuri na timu.

Hivi vilabu vyetu vya Simba na Yanga miaka nenda vimedumaa kwa sababu ya kuendekeza watu wenye fedha badala ya kutengeneza mfumo mzuri waa kuifanya timu kujitegemea!

Walipita watu kama Abbas Gulamali, Francis Kifukwe, Yusuf Manji (Yanga) na akina Azim Dewji, Kassim Dewji, na huyu Mohamed Dewji (Simba) ambao wamekuwa na desturi ya kuzijengea umaarufu hizi timu kupitia fedha zao, ila mwisho wa siku wanapo ondoka, timu zinayumba na kurudi nyuma kilometa kadhaa!

Siyo jambo zuri kuona Mwekezaji anakataa wawekezaji wengine kwenye timu. Yeye ana uwezo gani wa kuihudumia hiyo timu? Timu za wenzetu mfano Arsenal, Chelsea, nk. Zinamilikiwa na Matajiri! Lakini bado kila siku wanaingia mikataba na Makampuni mengine.

Mo anatakiwa kuishauri Bodi na hao Sportpesa namna ya kuboresha huo mkataba wao ili uendelee kuwa na maslahi kwa pande zote mbili! Ila siyo kuanzisha maneno ya fitna na majungu. Siku akijitoa Simba kama alivyofanya Yusuf Manji kule Yanga, timu itayumba.
 
Msaada ndugu ni lini hizi timu ziliwahi fanikiwa bila hawa Waasia?
 
Msaada ndugu ni lini hizi timu ziliwahi fanikiwa bila hawa Waasia?
Ndiyo maana hizi timu zetu kongwe zinatakiwa kutengeneza mifumo imara ya kujitegemea! Na siyo kumtegemea mtu mmoja. Yaani mashabiki wa Simba na Yanga hatutakiwi kuwashabikia hawa Wahindi kwa nguvu zetu zote!

Tuwe nao makini! Wengi wao kuanzia Abbas Gulamali, Yusuf Manji, Azim Dewji na sasa huyu Mo Dewji! Wana agenda zao za kujinufaisha wa kama wao, nyuma ya pazia. Na baadae wakitoka, unakuta timu imekua maskini ya kutupwa.
 
...Mohamed Dewji Mo utawadanganya mashabiki wa Simba kwa muda tu ila muda utafika ukweli wote utakuwa hadharani na wataona ujanja-ujanja wake na namna anavyoinyonya timu ya Simba.
Acha ampe changamoto SportPesa ili waongeze dau, ushindani wa udhamini hupandisha mafao. Sasa ulitaka SportPesa asipewe changamoto kwa kuwa hawakukutana barabarani?
 
Kimsingi Mo anatakiwa kuwa muwazi! Kama anaona Sportpesa wanatoa dau dogo, aahidi mbele ya Bodi ya Timu angetoa kiasi gani kama mdhamimi mkuu badala ya hao Sportpesa!
Inaelekea haujahifahamu stori iliyopelekea uzi huu kuanzishwa ndio maana unamtaja Mo kama 'mdhamini'. Nakushauri uitafute stori kwanza, uisome na kuielewa, then ndio uje kusoma na kuchangia uzi huu. Mo sio mdhamini, Mo ni mwekezaji ambaye naye anatafuta wadhamini sambamba na wanahisa wengine. Kuhusu kuwa muwazi kama SportPesa wanatoa dau dogo, katika stori hiyo ninayokwambia uitafute, utakuta ameandika kwa uwazi na takwimu kuonyesha udogo wa dau la SportPesa. Ni vizuri kusoma au kuwa informed kabla ya kuongea
 
Uyu alikuwa mtangazaji wa earadio,alifukuzwa kwasababu ya kukosa weredi.
 
Mishahara ya wachezaji wa Simba inalipwa na Sportpesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…