Simba, Sportpesa hawakukutana barabarani

Simba, Sportpesa hawakukutana barabarani

YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU yakamilisha Mchango wake wa milioni moja kwenda katika timu ya yanga:
:
Na
Yangawhatsapp_makaomakuu
:
:
Katika Kukamilisha Malengo Ya Kocha wa Yanga Mwinyi zahera
Na kamati ya Uchangishaji Michango Ya Yanga inayongozwa Na Mh Mavunde Leo Group la YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU,
:
Chini ya Mwenyekiti Wa Kamati Ya Fedha na uhamasishaji Ya Group Hilo Mussa Muro Amewashukuru Wanachama Wa group Kwa mchango Wao Kwa Klabu ya yanga wa Milioni Moja kwenda katika Akaunt ya Mwalimu Zahera kupitia Benk ya CRDB,
:
:
Akiwashukuru wanachama hao Mussa Muro amesema
Kwa niaba ya Uongozi YWSMM.
:
"Napenda kuwashukuru wanachama wetu wote tuliopambana na kujitolea katika kuichangia club yetu pendwa Young Africans Sc, ambayo kwetu imekuwa Kama imani. Ni moja ya sehemu kuu ya furaha katika maisha yetu.; Amesema Murro
:
Pia Murro Ameongezea maneno yafwatayo
:
"Tumechagua kuwa Yanga na Tunaipenda Yanga na tutaendelea kuipigania siku zote"
:
:
Ikumbukwe kampeni hii Ilizinduliwa Mkoani Dodoma Na Watu mbali mbali kukabiziwa Kadi za mchango Na magroup ya Whatsapp Baazi nayo Kupewa kadi hizo na Leo Group la YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU limejumuika na Magroup Mengine Katika Kukamilisha malengo ya klabu.
#SisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm[emoji1241]View attachment 1082422

Swali zuri sana atueleze Simba inanyonywa vipi na Mo,
Huyu Bw.Mdogo ni Kiongozi wa Ndani ya Yanga na amekuwa akipitisha bakuri na Michango Haramu ya kuwahonga akina Kambuzi. Mpuuuzeni kama Watopolo wengine. Mbaya zaidi wengine tunamjua majina na mpaka na anapoishi. Leo tu hapa jukwaa la Michezo anazo nyuzi 3 zinazoishambulia Simba na MO kwa ujumla. Tunakuonya wewe Bw.Mdogo habari za Simba waachie wenye timu yao utakuja kutoka jasho la MENO!
 
[emoji1428][emoji1428]Kuna wakati unaweza kufikiri kuwa unapofanikiwa kimaisha basi unafanikiwa pia kuwa na busara na hekima.

[emoji3499]Unadhani kabisa busara na hekima hizo, ni sawasawa na mafanikio uliyonayo, kumbe sivyo kabisa na hapa ndipo inakuja kauli ya inategemea utashi wa mtu na mtu.

[emoji3504]Wakati mchakato wa Mohammed Dewji 'Mo' kumiliki asilimia 49 za umiliki wa klabu ya Simba ukiwa haujakamilika yeye tayari anaruka na kutaka kupora madaraka na nguvu ya wanachama wenye hisa nyingi yaani Majority Share Holders

[emoji96]Wanachama wa Simba - chini ya Mwenyekiti, Bw. Mangungu wanamiliki hisa asilimia 51 zao klabu pale mchakato utakapokamilika.

[emoji731]Unaweza kurejea kwenye miongoni mwa maelekezo ya Tume ya Ushindani (FCC) waliyatoa kwa kusema kuwa mchakato uliotumika katika hatua za awali za kuelekea kwenye mabadiliko haukuwa wa kiungwana yaani Fair kwani kuna baadhi ya mambo yalikiukwa kisheria ama iwe kwa makusudi au bahati mbaya.[emoji1543][emoji1543]

[emoji851]Wakati mkataba kati ya Simba SC na Sportpesa ukiwa haujaisha huku wadhamini hao wakiendelea kutimiza majukumu yao ya kimkataba anatokea Mohamed Dewji Mo na kauli zake.

[emoji451]Mo ambaye yuko kwenye mchakato wa kumiliki hisa asilimia 49 na kuanza kukejeri na kushusha thamani ya Sportspesa inayofanya makubwa katika kuinua soka la ukanda wetu wa Afrika mashariki na kati.

[emoji736]Nani asiyejua nguvu ya kipesa na uwekezaji ya sportpesa[emoji780][emoji780]

[emoji687]Hii ni kampuni ambayo ilianza kujishughulisha na maswala ya soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati kwa zaidi ya miaka saba sasa.

[emoji3519]Juhudi wanazofanya katika kuendeleza soka letu kwa kudhamini timu zetu kubwa tena kwa kipindi cha miaka 5 halafu anatokea mtu mwenye ulafi na uroho wa kuwanyonya Wanasimba na wapenda soka na kuanza dhihaka.

[emoji703]Simba imepitia vipindi vigumu sana kuna kipindi hata usajili na misahara ilikuwa shida na kupelekea migogoro ya kila namna leo hii anatokea mtu na kukebehi.

[emoji751]Maendeleo ni hatua wanapoanza wenzako maana yake wanatengeneza njia nzuri kwako uwezi kubeza juhudi ambazo zimekufanya leo uikute timu hapa ilipo.

[emoji302] Kama unaweza kulinganisha thamani ya mkataba wa Manchester United ambao wamesaini kwa zaidi ya Sh bilioni 700 huku wewe mpaka leo unakwepa kuweka Sh. bilioni 20 tu kwenye akaunti ya Simba ni zaidi ya ukichaa, kutokuelewa kwamba wewe ni mbabaishaji

[emoji1415]Mohamed Dewji Mo aliwahi kudhamini timu zaidi ya moja ikiwemo African Lyon na Singida United ambako alishindwa vibaya na kuja kujipenyeza Simba kwa kufuata mtaji wa mashabiki wengi.

[emoji49]Katika ndoa isiyo rasmi kati yake na Simba, yeye ndiye mnufaikaji kwa kuwatumia watu wake ambao amewapa nafasi ndani ya Simba ili wafanye madudu kwa malengo ya kupata faida.

[emoji1754]Ndiyo maana leo hii ameanzisha Simba zaidi ya 5 ili kutumia nguvu ya mashabiki wa Simba kama mtaji kwenye biashara zake.

[emoji1476]Swali rahisi na jepesi Simba sc ndio walioingia mkataba na Sportpesa miaka mitano iliyopita ambako Juni, mwaka huu ndio unafikia tamati kwa kufungua mlango wa majadiliano baina ya pande mbili ili kuona waendelee au lah.

[emoji1602]Tumeshuhudia kampuni mbalimbali kama Vodacom, Serengeti, NMB na mengine mengi kwa nyakati tofauti yakiingia udhamini uwe na klabu au Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

[emoji1421]Na punde pande mbili zinaposhindwa kuendelea, huachana kiungwana na kutafuta udhamini mpya bila kashfa wala mizingwe. Huo ndio ustarabu wa kibiashara na ushindani.

🤏[emoji2535]Kwa alichokifanya Mohamed Dewji Mo kwa Mdhamini Mkuu wa Simba sc Sportpesa ni kitendo ambacho kimekosa weledi na ile kauli ya Tume ya FCC inaonekana nguvu yake.

[emoji188]Ni wakati wa Mangungu - Mwenyekiti wa Simba kutoa kauli ya kupinga maneno ya Mohamed Dewji Mo kwa kuitumia klabu katika harakati zake za kutafuta namna ya kujipenyeza ili aendelee kuwanyonya Wanamsimbazi.

[emoji89]Kinyume na hapo itatujengea wakati mgumu na kufanya kampuni kubwa kusita kujitokeza na kuwekeza kwenye klabu zetu kwani zipo klabu zinazitamani kupata udhamini kama ambao Simba wameendelea kupatiwa.

[emoji1532][emoji1532]Huku akikebehi Sportpesa,Machi 30 mwaka huu, Simba watapokea hundi ya malipo ya mishahara ya wachezaji kutoka Sportpesa.

[emoji1745][emoji2535]‍[emoji3603]Mohamed Dewji Mo utawadanganya mashabiki wa Simba kwa muda tu ila muda utafika ukweli wote utakuwa hadharani na wataona ujanja-ujanja wake na namna anavyoinyonya timu ya Simba.

[emoji102][emoji102]Nitakaporudi nitakuja na maneno yako ya kupewa.[emoji147][emoji147]

Msemakweli wa haki

Nimemaliza
Umeandika hoja yenye mashiko sana mtoa mada. Ila ni jambo la kushangaza mashabiki wa timu husika wanakimbilia tu kukukejeli na kukutupia kila aina ya maneno ya karaha!

Nakumbuka sana enzi zile timu zetu hizi mbili zilipokuwa mahututi huku Gor Mahia ya Kenya ikifaidi matunda ya hawa jamaa Sportpesa, kabla ya hao Sportpesa kuingia Bongo na kutoa udhamini ambao umezisaidia sana hizi klabu zetu mbili (Yanga na Simba)

Kimsingi Mo anatakiwa kuwa muwazi! Kama anaona Sportpesa wanatoa dau dogo, aahidi mbele ya Bodi ya Timu angetoa kiasi gani kama mdhamimi mkuu badala ya hao Sportpesa! Tofauti na hapo, ataonekana ana majungu na hana nia nzuri na timu.

Hivi vilabu vyetu vya Simba na Yanga miaka nenda vimedumaa kwa sababu ya kuendekeza watu wenye fedha badala ya kutengeneza mfumo mzuri waa kuifanya timu kujitegemea!

Walipita watu kama Abbas Gulamali, Francis Kifukwe, Yusuf Manji (Yanga) na akina Azim Dewji, Kassim Dewji, na huyu Mohamed Dewji (Simba) ambao wamekuwa na desturi ya kuzijengea umaarufu hizi timu kupitia fedha zao, ila mwisho wa siku wanapo ondoka, timu zinayumba na kurudi nyuma kilometa kadhaa!

Siyo jambo zuri kuona Mwekezaji anakataa wawekezaji wengine kwenye timu. Yeye ana uwezo gani wa kuihudumia hiyo timu? Timu za wenzetu mfano Arsenal, Chelsea, nk. Zinamilikiwa na Matajiri! Lakini bado kila siku wanaingia mikataba na Makampuni mengine.

Mo anatakiwa kuishauri Bodi na hao Sportpesa namna ya kuboresha huo mkataba wao ili uendelee kuwa na maslahi kwa pande zote mbili! Ila siyo kuanzisha maneno ya fitna na majungu. Siku akijitoa Simba kama alivyofanya Yusuf Manji kule Yanga, timu itayumba.
 
Msaada ndugu ni lini hizi timu ziliwahi fanikiwa bila hawa Waasia?
 
Msaada ndugu ni lini hizi timu ziliwahi fanikiwa bila hawa Waasia?
Ndiyo maana hizi timu zetu kongwe zinatakiwa kutengeneza mifumo imara ya kujitegemea! Na siyo kumtegemea mtu mmoja. Yaani mashabiki wa Simba na Yanga hatutakiwi kuwashabikia hawa Wahindi kwa nguvu zetu zote!

Tuwe nao makini! Wengi wao kuanzia Abbas Gulamali, Yusuf Manji, Azim Dewji na sasa huyu Mo Dewji! Wana agenda zao za kujinufaisha wa kama wao, nyuma ya pazia. Na baadae wakitoka, unakuta timu imekua maskini ya kutupwa.
 
...Mohamed Dewji Mo utawadanganya mashabiki wa Simba kwa muda tu ila muda utafika ukweli wote utakuwa hadharani na wataona ujanja-ujanja wake na namna anavyoinyonya timu ya Simba.
Acha ampe changamoto SportPesa ili waongeze dau, ushindani wa udhamini hupandisha mafao. Sasa ulitaka SportPesa asipewe changamoto kwa kuwa hawakukutana barabarani?
 
Kimsingi Mo anatakiwa kuwa muwazi! Kama anaona Sportpesa wanatoa dau dogo, aahidi mbele ya Bodi ya Timu angetoa kiasi gani kama mdhamimi mkuu badala ya hao Sportpesa!
Inaelekea haujahifahamu stori iliyopelekea uzi huu kuanzishwa ndio maana unamtaja Mo kama 'mdhamini'. Nakushauri uitafute stori kwanza, uisome na kuielewa, then ndio uje kusoma na kuchangia uzi huu. Mo sio mdhamini, Mo ni mwekezaji ambaye naye anatafuta wadhamini sambamba na wanahisa wengine. Kuhusu kuwa muwazi kama SportPesa wanatoa dau dogo, katika stori hiyo ninayokwambia uitafute, utakuta ameandika kwa uwazi na takwimu kuonyesha udogo wa dau la SportPesa. Ni vizuri kusoma au kuwa informed kabla ya kuongea
 
Huyu Bw.Mdogo ni Kiongozi wa Ndani ya Yanga na amekuwa akipitisha bakuri na Michango Haramu ya kuwahonga akina Kambuzi. Mpuuuzeni kama Watopolo wengine. Mbaya zaidi wengine tunamjua majina na mpaka na anapoishi. Leo tu hapa jukwaa la Michezo anazo nyuzi 3 zinazoishambulia Simba na MO kwa ujumla. Tunakuonya wewe Bw.Mdogo habari za Simba waachie wenye timu yao utakuja kutoka jasho la MENO!
Uyu alikuwa mtangazaji wa earadio,alifukuzwa kwasababu ya kukosa weredi.
 
Mishahara ya wachezaji wa Simba inalipwa na Sportpesa?
 
Back
Top Bottom