moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
[emoji1428][emoji1428]Kuna wakati unaweza kufikiri kuwa unapofanikiwa kimaisha basi unafanikiwa pia kuwa na busara na hekima.
[emoji3499]Unadhani kabisa busara na hekima hizo, ni sawasawa na mafanikio uliyonayo, kumbe sivyo kabisa na hapa ndipo inakuja kauli ya inategemea utashi wa mtu na mtu.
[emoji3504]Wakati mchakato wa Mohammed Dewji 'Mo' kumiliki asilimia 49 za umiliki wa klabu ya Simba ukiwa haujakamilika yeye tayari anaruka na kutaka kupora madaraka na nguvu ya wanachama wenye hisa nyingi yaani Majority Share Holders
[emoji96]Wanachama wa Simba - chini ya Mwenyekiti, Bw. Mangungu wanamiliki hisa asilimia 51 zao klabu pale mchakato utakapokamilika.
[emoji731]Unaweza kurejea kwenye miongoni mwa maelekezo ya Tume ya Ushindani (FCC) waliyatoa kwa kusema kuwa mchakato uliotumika katika hatua za awali za kuelekea kwenye mabadiliko haukuwa wa kiungwana yaani Fair kwani kuna baadhi ya mambo yalikiukwa kisheria ama iwe kwa makusudi au bahati mbaya.[emoji1543][emoji1543]
[emoji851]Wakati mkataba kati ya Simba SC na Sportpesa ukiwa haujaisha huku wadhamini hao wakiendelea kutimiza majukumu yao ya kimkataba anatokea Mohamed Dewji Mo na kauli zake.
[emoji451]Mo ambaye yuko kwenye mchakato wa kumiliki hisa asilimia 49 na kuanza kukejeri na kushusha thamani ya Sportspesa inayofanya makubwa katika kuinua soka la ukanda wetu wa Afrika mashariki na kati.
[emoji736]Nani asiyejua nguvu ya kipesa na uwekezaji ya sportpesa[emoji780][emoji780]
[emoji687]Hii ni kampuni ambayo ilianza kujishughulisha na maswala ya soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati kwa zaidi ya miaka saba sasa.
[emoji3519]Juhudi wanazofanya katika kuendeleza soka letu kwa kudhamini timu zetu kubwa tena kwa kipindi cha miaka 5 halafu anatokea mtu mwenye ulafi na uroho wa kuwanyonya Wanasimba na wapenda soka na kuanza dhihaka.
[emoji703]Simba imepitia vipindi vigumu sana kuna kipindi hata usajili na misahara ilikuwa shida na kupelekea migogoro ya kila namna leo hii anatokea mtu na kukebehi.
[emoji751]Maendeleo ni hatua wanapoanza wenzako maana yake wanatengeneza njia nzuri kwako uwezi kubeza juhudi ambazo zimekufanya leo uikute timu hapa ilipo.
[emoji302] Kama unaweza kulinganisha thamani ya mkataba wa Manchester United ambao wamesaini kwa zaidi ya Sh bilioni 700 huku wewe mpaka leo unakwepa kuweka Sh. bilioni 20 tu kwenye akaunti ya Simba ni zaidi ya ukichaa, kutokuelewa kwamba wewe ni mbabaishaji
[emoji1415]Mohamed Dewji Mo aliwahi kudhamini timu zaidi ya moja ikiwemo African Lyon na Singida United ambako alishindwa vibaya na kuja kujipenyeza Simba kwa kufuata mtaji wa mashabiki wengi.
[emoji49]Katika ndoa isiyo rasmi kati yake na Simba, yeye ndiye mnufaikaji kwa kuwatumia watu wake ambao amewapa nafasi ndani ya Simba ili wafanye madudu kwa malengo ya kupata faida.
[emoji1754]Ndiyo maana leo hii ameanzisha Simba zaidi ya 5 ili kutumia nguvu ya mashabiki wa Simba kama mtaji kwenye biashara zake.
[emoji1476]Swali rahisi na jepesi Simba sc ndio walioingia mkataba na Sportpesa miaka mitano iliyopita ambako Juni, mwaka huu ndio unafikia tamati kwa kufungua mlango wa majadiliano baina ya pande mbili ili kuona waendelee au lah.
[emoji1602]Tumeshuhudia kampuni mbalimbali kama Vodacom, Serengeti, NMB na mengine mengi kwa nyakati tofauti yakiingia udhamini uwe na klabu au Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
[emoji1421]Na punde pande mbili zinaposhindwa kuendelea, huachana kiungwana na kutafuta udhamini mpya bila kashfa wala mizingwe. Huo ndio ustarabu wa kibiashara na ushindani.
🤏[emoji2535]Kwa alichokifanya Mohamed Dewji Mo kwa Mdhamini Mkuu wa Simba sc Sportpesa ni kitendo ambacho kimekosa weledi na ile kauli ya Tume ya FCC inaonekana nguvu yake.
[emoji188]Ni wakati wa Mangungu - Mwenyekiti wa Simba kutoa kauli ya kupinga maneno ya Mohamed Dewji Mo kwa kuitumia klabu katika harakati zake za kutafuta namna ya kujipenyeza ili aendelee kuwanyonya Wanamsimbazi.
[emoji89]Kinyume na hapo itatujengea wakati mgumu na kufanya kampuni kubwa kusita kujitokeza na kuwekeza kwenye klabu zetu kwani zipo klabu zinazitamani kupata udhamini kama ambao Simba wameendelea kupatiwa.
[emoji1532][emoji1532]Huku akikebehi Sportpesa,Machi 30 mwaka huu, Simba watapokea hundi ya malipo ya mishahara ya wachezaji kutoka Sportpesa.
[emoji1745][emoji2535][emoji3603]Mohamed Dewji Mo utawadanganya mashabiki wa Simba kwa muda tu ila muda utafika ukweli wote utakuwa hadharani na wataona ujanja-ujanja wake na namna anavyoinyonya timu ya Simba.
[emoji102][emoji102]Nitakaporudi nitakuja na maneno yako ya kupewa.[emoji147][emoji147]
Msemakweli wa haki
Nimemaliza