Tetesi: Simba Sports Club kuhamia ligi ya Zanzibar mwakani: Move imeanza

Tetesi: Simba Sports Club kuhamia ligi ya Zanzibar mwakani: Move imeanza

Hizo bangi unazovuta uziache zitakufanya uokote makopo muda sio mrefu, yani Simba itoke ligi ya bongo ikahamie kwa wanywa urojo wa chambawima 🤔🤔 acha bangi wewe
 
kama ni msimu ujao tunamshukuru mungu kwamba tutamalizia ile mechi yetu ya mkondo wa pili tuwaage watani...kila la kheri muendako...sijawahi waza kama ntakuja shabikia timu ambayo inagawa vichapo mpk timu pinzani zinawakimbia,kuna kipindi hata barcelona walitaka wakimbie la liga nikaona hawa wanaikimbia madrid yangu hawa kkkkkkkkkk
 
Za ndani saana, utaribu wa mageuzi makubwa ya kimpira utaanza baada ya dirisha dogo January. Club kubwa barani afrika inameanza hatua mahsusi za kuweka base kubwa ya kimpira visiwani Zanzibar.

Kandarasi hii na maamuzi haya yanakuja baada ya kubaini kuwa kuna wahuni wanaharibu mpira bara na hakuna anaeshuhulika nao kwa mana ya kudhibiti takataka zinazoendelea. Kikao cha usiku wa manane kimependekeza kuwa msimu ujao ni Zanzibar na kinaandaa taratibu za kualika timu zifuatazo katika ligi hiyo ya Zanzibar 1. Al hilal Omduman, Al merlek, Gormahia, Tasker, APR na Vital O ya Burundi.

Dhumuni la uamuzi huu ni kutimiza ndoto za kimashindano pasipo uswahili, kuchanganya mpira na siasa na maslahi ya wahuni wachache.

Nimekaa paleee mtaikumbuka post hii
Viongozi wa Zanzibar tokea maponduzi ni Yanga laugh 🤣 na kwakuwa lawama za kufungwa mara nne mfululizo wameipa serikali ya CCM basi ni bora waamie ligi ya Burundi au ya Kenya, huko CCM haina influence.
 
Wanasimba lazima tutambue tu, Yanga ni kama maji, lazima tutakutana naye tu hata tukihamia Zanzibar.
 
Ni kweli kwamba sikubaliani na baadhi ya vitu kwenye ligi yetu lakini kufikiria kuhamisha timu ni uboya.
Viongozi wa simba acheni vitisho vya kishamba.
Tupambane hapa hapa mpaka tufikie malengo yetu.
Kabla hamjahama tukipige kimoja cha kuagana na Yanga
 
Back
Top Bottom