SI KWELI Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union

SI KWELI Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Salaam Wakuu,

Ikiwa Ligi Kuu ya NBC imeisha leo 28/05/2024 huku Yanga akiwa Bingwa Azam nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu. Kuna tetesi kuwa Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union. Taarifa hiyo inadai Kombe la Shirikisho limefutwa.

Je, kuna ukweli wowote wa taarifa hii?

1716923060043.png
 
Tunachokijua
Tanzania ni miongoni mwa nchi inayotaraji kuwa na Uwakilishi wa timu 4 katika michuano ya CAF ya mwaka 2024/2025. Utaratibu wa kushiriki michuano ya CAF unaangalia nafasi nne za juu kwenye ligi husika, Timu inayoshika nafasi ya kwanza na ya pili zinashiriki michuano ya ligi ya Mabingwa huku zilizoshika nafasi ya tatu na ya nne wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Ligi ya Tanzania (Ligi Kuu ya NBC) ya Msimu wa 2023/24 imemalizika rasmi mnamo 28/05/2024 huku Yanga wakiibuka Mabingwa, Azam wameshika nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu na Coastal Union nafasi ya nne. Kwa kutokana na msimamo ulivyo kwa taratibu za msimu wa 2023-24 Yanga na Azam zinakuwa zimefuzu kucheza ligi ya Mabingwa wakati Simba na Coastal Union zinakuwa zimefuzu kucheza Kombe la Shirikisho.

Baada ya kumalizika kwa Ligi ya Tanzania (Ligi Kuu ya NBC) ya Msimu wa 2023/24 imeibuka taarifa inayodai kwamba Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union. Taarifa hiyo inadai Kombe la Shirikisho limefutwa. Taarifa hii ilianza kuibuka kabla ya ligi kumalizika (Soma hapa), na ikashika kasi zaidi siku ya Mei 28, 2024 baada ya kuwekwa na Mwandishi wa Habari ya michezo Nassib Mkomwa katika ukurasa wake wa Instagram (Soma hapa).

Upi ukweli wa taarifa hii?
Katika kutafuta uhakika wa taarifa hii JamiiCheck imefanya mawasiliano na Nassib Mkomwa pamoja na Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo kupata uhalisia wa taarifa hii.

Kwa upande wake Nassib Mkomwa anasema kuwa habari hii ni ya ndani ya CAF bado haijatoka rasmi, bado majadiliano yanaendelea na haujafikiwa muafaka. Taarifa hizi alipewa na mtu wa ndani wa Simba. Akieleza hoja hiyo Nassibu Anasema:

Hizo ni taarifa za ndani, hazipatikani mtandaoni wala kwenye vyanzo kwa kuwa bado hazijatoka ndio kwanza zipo katika mchakato.
Mimi nimeambiwa na mshkaji wangu ambaye yupo Simba, amesema huo mchakato unafanyika ila bado hawajafikia muafaka, wanafanya mikutano. Ameniambia wanataka kuongeza timu kwa kuwa michuano ya Kombe la Shirikisho wanasema haina hela sana, hivyo mpango ni kuongeza timu ili kuongeza kipato.
Hoja ya Nassib Mkomwa inaonesha kuwa habari hii ameitoa ndani na bado haijatoka nje sababu maamuzi hayajafanywa. Kwa msingi huu inaonesha taarifa aliyoitoa haina uhakika.

Katika kujiridhisha zaidi, JamiiCheck ilipitia Kurasa zote za CAF Hii, Hii na hii lakini hakuna taarifa yoyote inayoeleza kufutwa kwa Michuano ya Kombe la Shirikikisho sababu ya michuano ya Kombe Ligi ya Afrika African Football League. Hoja hii pia inasaidia kufifisha madai ya kuwepo uwezekano wa Michuano ya Shirikisho kufutwa sababu ni hatua kubwa ambayo haijatolewa mahali popote katika kurasa rasmi za Shirikisho la soka la Afrika CAF.

JamiiCheck ilijiridhisha zaidi kwa kuwasiliana na Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo ambaye amekanusha taarifa ya inayodai Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union. Taarifa hiyo inadai Kombe la Shirikisho limefutwa.

Akiifafanulia JamiiCheck Ndimbo anasema:
Hakuna kitu kama hicho, ukiangalia hata kwenye msimamo wetu wa ligi unaonesha wawili watakaocheza Ligi ya Mabingwa. Kukiwepo na utaratibu mwingine tutawajuza. Hiyo African Football League, ipo kama ilivyokuwa ile iliyopita.
Majibu ya Cliford Ndimbo yanaendana na Majibu ya Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kasongo Almasi Kasongo ambaye amekanusha kufutwa michuano ya Kombe la Shirikisho na kudai timu nne zitacheza michuano ya CAF huku walioshika nafasi mbili za juu watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na nafasi ya tatu na nne watacheza Shirikisho.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo hapo juu JamiiCheck imejiridhisha kuwa hoja inayodai kuwa Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union haina ukweli

Tunawasilisha na wenye mpira nadhani kesho watatupa jibu sahihi.
 
Back
Top Bottom