Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
- Thread starter
-
- #1,261
Amesema yeye ni mnyama lakini alikuwa anaiunga mkono team ya FC
Wana Simba samahanini kwa ukimya sababu simu iliniishia chaji ila Leo nimefarijika sana kwani baada ya mgomo baridi ambao ulikuwa unaelekea kunukia vurugu kwa watu kugoma kuingia uwanjani kushinikisha kiingilio ni kikubwa mno ila baada ya mda wa masaa takribani mawili mapenzi ya dhati toka moyoni yakachukua nafasi kwa watu kukubali kuchangia timu yao Simba kwa kukubali kulipa Tsh 5000 badala ya Tsh3000.
Kingine kilichoacha uwanja ukiwa na shangwe nyingi ni G. Lema uku akiondoka na mashabiki uku wakiivisha gari lake bendera ya Simba kwenye ile chuma inayokaa bendera ndogo ya serikali.
Mungu ibariki Simba
Moto ni ule ule mpaka kwa TP MAZEMBE.
Viva SIMBA
TP mazembe wanashuka dimbani kesho kuikabili simba huku wachezaji wake wakionyesha kusumbuliwa na uchovu baada ya kucheza mechi nyingi msimu huu.
Source:mwanaspot.co.tz
Acha watanzania wajipe matumaini. Huo uchovu ndio uliowapa Sofapaka burungutu la 9 - 0 kutoka kwa hao TP Mazembe.
Kila la heri Simba. Ila mfahamu kwamba mna kazi kubwa sana hasa ukizingatia hamjapata international friend match hata moja, na mechi ya mwisho ilikuwa dhidi ya AFC ya Arusha. So kuna dalili za wazi za kifungwa kuliko vinginevyo.
mkuu hapa hakuna wasiwasi wowote,hawa TP mazembe mpaka sasa hivi tushawapiga , wachezaji wetu wapo fit kisaikologically na fizikali...hawa TP nimeangalia website zao wanatuogopa sana kutokana na historia yetu,, wanajua tushawahi kuwapiga Zamaleki...wao wenyewe wanajua kuwa mziki wetu si wa kitoto kabisa.
Mkuu, kama kweli hayo unayoongea ndo yapo vichwani mwa wachezaji wa Simba na viongozi wao, basi mtafungwa vibaya sana maana inaonyesha wazi wameshawafunga kisaikolojia pia. Yaani kweli unathubutu kuamini kinachoandikwa ktk web yao? Eti muziki wetu sio wa kitoto, kwa kutoka sare na Yanga na kuifunga AFC mbili bila??? Hivi kweli na wewe unaamini Mazembe wanawaogopa??? Yaani kuitoa Zamalek miaka kibao iliyopita ndio cha kuwatisha TP? Pole sana mkuu najua wewe ni mmoja wa watanzania walioathirika vibaya na soka la mdomoni, ila maandalizi ZERO! Tusubili tuone "MZIKI " wenu kesho ila usipotee kesho, uje tena hapa
Kikosi kitakachoshuka kesho:
Juma kaseja, Haruna Shamte,Amir Mafta,Kelvin Yondani,Juma Nyosso,Jerry Santo,Rashid Gumbo/Niko Nyagawa,Patrick Ochan,Emanuel Okwi, Mbwana Samata,Amri Kiemba
Kikosi kitakachoshuka kesho:
Juma kaseja, Haruna Shamte,Amir Mafta,Kelvin Yondani,Juma Nyosso,Jerry Santo,Rashid Gumbo/Niko Nyagawa,Patrick Ochan,Emanuel Okwi, Mbwana Samata,Amri Kiemba
Ktk lineup hiyo nadhani Kaseja kama vile kachuja .... bora golini akae Bathez