Simba sports club yatenga bajeti kabambe mashindano ya kimataifa

Simba sports club yatenga bajeti kabambe mashindano ya kimataifa

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Simba imetangaza bajeti ya Sh6.1 bilioni kwa msimu huu 2019/2020 katika kuhakikisha klabu hiyo itatetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kurudi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Bajeti hiyo ilitajwa kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

Katika bajeti hiyo, klabu ya Simba imetenga Sh76.8 Milioni za usajili wa dirisha dogo utakaoanza hivi karibuni.

Mbali na usajili wa dirisha dogo, klabu ya Simba itatumia Sh 4.16 Bilioni kwa ajili ya mishahara ya wachezaji na Sh 408 kwa ajili ya bonusi.

Katika bajeti hivyo, vyanzo vya mapato vitaiingizia klabu ya Simba Sh 5.814 Bilioni ambayo ni pungufu ya Sh373 milioni katika mapato ya klabu.

Chanzo: Mwananchi
 
Big timu langu, songa mbele hii ni level ya kimataifa zaidi na sio ya kata kama.wale madimbwini complex
 
Simba wafanye yoooote lakini msingi mkubwa wa kujitangaza na kujiuza kama club na kama brand wafanye vizuri uwanjani na mambo mengine yatafuatia
 
M. 76.8 si mchezaji mmoja tu, tena wa humu humu bongo! Kwa hela hiyo hata Molinga Ndama Falcao hamumpati!
 
kwa hiyo hao wachezaji watakaosajili kwa milioni 70 ndio watashindana na TP MAZEMBE, AK AHLY, WYDAD CASABLANCA? hahaha
19/20 simba ilishatolewa champions league mkuu, na huo usajili ni dirisha dogo linalo funguliwa mwezi huu
 
Back
Top Bottom