Simba taarifa walipewa na nani kuwa mechi itachezwa uwanja wa Mkapa?

danhoport

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
2,116
Reaction score
4,885
Nataka kujua tu sio kwa ubaya, yaani ilikuwaje mpaka wakatangaza viingilio na kuanza kuuza tiketi. Taarifa walipewa na nani?
 
Huu muda ungeutumia kuchomoa mwiko nyuma ili siku game Pale kwa mkapa ukae vizuri kushudia mnyama akichukua kombe kibabe sana
 
Huu muda ungeutumia kuchomoa mwiko nyuma ili siku game Pale kwa mkapa ukae vizuri kushudia mnyama akichukua kombe kibabe sana
Kwa mkapa gani tena au nawe umemsikiliza familia Karia
 
Nataka kujua tu sio kwa ubaya, yaani ilikuwaje mpaka wakatangaza viingilio na kuanza kuuza tiketi. Taarifa walipewa na nani?

Kawaida timu mwenyeji kupitia chama/shirikisho la mpira la nchi huwa inatoa taarifa CAF juu ya uwanja upi itatumia...

CAF wao wanadhibitisha au pendekeza uwanja mwingine kama uwanja uliotajwa awali hauendani na standards zao...

Simba itakuwa walijiaminisha kuwa Ben Mkapa utakuwa fresh kutokana na kauli za kina Mwan FA na Msigwa...

Na pia hata ukitazama kwa mechi ya Al Masry, uwanja ulikuwa vibaya kwenye pitch kuliko sasa, ni dhahiri pia Simba kwa 100% walijua tu piga ua garagaza boli la fainali lazima litembee kwa Mkapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…