Simba tafuteni uwanja wenye taa Kwa mechi za katikati ya wiki

Equalise

Senior Member
Joined
Oct 8, 2024
Posts
111
Reaction score
269
Hata kule ulaya mechi za katikati ya wiki huwa zinachezwa usiku tofauti na za week end ili kuwapa mashabiki wengi kuburudika.Sasa nyinyi mechi za katikati ya wiki mnacheza saa kumi jioni hii mnapelekea kujipunguzia mapato na kuwanyima burudani mashabiki wengi Kutokana na muda huo kuwa vibaruani.

Angalau saa 11 au 12 jioni sio mbaya Kwa muda huo mechi kuanza.
 
Mechi za katikati ya wiki zinatakiwa zichezwe kuanzia saa 3 usiku.
 
Dsm kuna uwanja gani? wenye taa zaidi ya chamazi ambao unatumiwa na Azam na yanga? unataka wahamie dodoma, manjaliwa ama kaitaba? Kwanza uwanja wa KMC upo mjini na ni mdogo ni rahisi kuujaza hata kwa iyo saa kumi na ukajaa, maana hata watu wa maofisi kama, posta, masaki, oystarbay, kinondoni, makumbusho, mikocheni, ubungo, msasani, tandale, sinza, kariakoo, mbezi,kawe, tegeta nk. maeneo yote tajwa hapa ni rahisi mno kufika mwenge uwanjani. Hoja yako haina mashiko.
 
Kwani chamazi hauwezi kutumiwa na zaidi ya timu mbili? Mbona uwanja WA Mkapa ulikuwa unatumiwa na timu tatu KMC, Simba , Yanga na muda mwingine Azam. Utetezi wako hauna mashiko Kwa kuona uwanja WA Azam hauwezi kutumiwa na Simba kisa Yanga na Azam wanautumia.
 
Kwa akili yako mtoa mada ni kwamba watu wote wameajiriwa!?
 
Dsm kuna uwanja gani? wenye taa zaidi ya chamazi ambao unatumiwa na Azam na yanga? unataka wahamie dodoma, manjaliwa ama kaitaba? Kwanza uwanja wa KMC upo mjini na ni mdogo ni rahisi kuujaza hata kwa iyo saa kumi na ukajaa, maana hata watu wa maofisi kama, posta, masaki, oystarbay, kinondoni, makumbusho, mikocheni, ubungo, msasani, tandale, sinza, kariakoo, mbezi,kawe, tegeta nk. maeneo yote tajwa hapa ni rahisi mno kufika mwenge uwanjani. Hoja yako haina mashiko.
Naunga mkonyo andiko lako
 
Sio lazima simba pia kutumia uwanja wa Azam kama KMC ground tunapata matokeo mazuri na pira linatembea, Ama ndio wivu tena? juzi kati mlikuja kutaka kuleta fitina na mitunguri yenu wazee wa kuruka ukuta.
 
Ni ushauri mzuri lakini sijui kama viongozi wa Simba watauzingatia. Wanaamini ushirikina kuliko kikosi chao walichosajili na benchi lao ufundi waliloliajiri. Waliniacha hoi pale walipopata matokeo mabovu Chamazi wakaamini wamelogwa wakaihamishia timu Mwenge.

Il nao wapanga ratiba si wangekuwa wana adjust ratiba walau hata mechi moja moja ya hizi timu kubwa iwe inaangukia kati ya jumamosi au jumapili kupunguza watu kutoroka vibaruani.
 
Back
Top Bottom