SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ni jambo jema kufanya mambo ya kusaidia jamii mfano kushiriki katika shughuli mbalimbali za ukusanyaji fedha kwa ajili ya maendeleo ya jamii hasa wale wenye uhitaji maalumu. Hivi sasa wakati timu zote zikiwa katika mapumziko, taasisi mbalimbali zikiwemo za wachezaji wameandaa mechi mbalimbali za kibonanza kwa ajili ya kukusanya fedha kuchangia shughuli mbalimbali.
Kawaida, professional teams wanawekaga utaratibu maalumu ukiwa na malengo ya kuhakikisha si tu mchezaji hapati majeraha lakini pia hadhi ya mchezaji na timu inalindwa na pia program nzima ya mapumziko ya wachezaji haiharibiwi. Katika fuatilia yangu nimeona baadhi ya haya mabonanza, pamoja na nia njema yanaweza yasiijenge wala kulinda hadhi ya taasisi ya Simba.
Tukumbuke Yanga wamekuwa vyema sana miaka hii miwili katika suala zima la marketing na publicity ambayo mara nyingi inafika katika level za propaganda. Pamoja na utani wa jadi, wote tumeshuhudia mara kadhaa upande ule wakitoa kauli za kudhalilisha au kushusha rekodi na mafanikio ya wachezaji, viongozi na klabu ya Simba na kutokana na nguvu kubwa wanayotumia hayo yote kuonekana sawa. Simba wamekuwa "too reactive" sana katika eneo hili na kuwaacha Yanga watambe wanavyotaka.
Leo hii unaenda kumchezesha Mzamiru dhidi ya Ali Kamwe, Kibu Mkandaji dhidi ya Hersi, hii haina afya kwa Simba. Uongozi inabidi uweke utaratibu na wapime kama kila bonanza ambayo wachezaji fulani wamealikwa, kama kweli maandalizi na washiriki wake vina hadhi inayoendana na brand ya Simba na kama kuna nia njema na pia kama ushiriki wao hautakuwa na athari yoyote kwa mchezaji na klabu kwa ujumla either kwa upande wa heshima au brand kiujumla. Kuna njia nyingi za kutoa sapoti na siyo lazima wachezaji kucheza, kuhudhuria tu pia ni sapoti kubwa.
Msiachie wachezaji wenu wanarandaranda hovyo kama watoto wa mitaani halafu kesho watu hao hao walioenda kuwapa sapoti watakuja kuwavunjia heshima. Tuache kuishi kinyonge.
Nadhani nimeeleweka.