MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Kuna kila dalili timu yetu imekuwa na underground management crisis ambayo kwa nje hatuoni. Ni vizuri tuamue hatma ya timu yetu sasa kabla haijawa worse zaidi next season.
Hii timu tulikubaliana iendeshwe kisasa lakini lazima tujue kuna watu wana maslahi yao "kiulaji" na pia mwekezaji ana mipango yake. Ni dhahiri mwekezaji ameshindwa kufanya mambo aliyoahidi kwa uwazi wa kutosha ili uwekezaji wake utoke kwenye masimulizi na tuone macho thamani ya huo uwekezaji.
Pia wale wazee wa maslahi ni dhahiri wakilamba asali wanamsifia mwekezaji lakini mirija ikikatwa ndio wanakumbuka kuwa Simba inahitaji kujitegemea!
Mpaka sasa inaonekana timu inamtegemea mtu badala ya kusimama yenyewe! Tunasema tayari tuna 20 bilioni lakini tunasajili wachezaji average ambao hawawezi kuifunga hata Geita Gold.
Haya mauza mauza ya timu ni moja ya sababu kuu ni uongozi kugawanyika na mara nyingi hii imetokea huko nyuma lakini kila mara inajirudia na ku resolve lakini inakuwa imeshaacha majeraha yasiyotibika.
Si kweli na huu uongo unaochagizwa hadi na wachambuzi kuwa daby ni daby hata uwe na timu bora kiasi gani! Huwezi kuwa na timu bora kiwango cha kushinda game za ndani na nje za kimataifa alafu usumbuliwe na Yanga! Tunahitaji wachezaji bora! Haina maana kuwa na professional player anayewekwa benchi na wazawa!
Wekeni sawa mambo yenu ya kiutawala na hasa uwazi wa uendeshaji wa timu. Tafuteni kocha bora mwenye historia ya makombe na anayejua soka la Afrika atumie uzoefu wake kuleta watu wa maana saba na kumbakisha Inonga, Chama na Bwalya tu.
Wekeni msingi wa uwazi ili kuondoa migogoro na kuturudisha enzi timu inaendeshwa kienyeji. Matatizo yote yameanzia huko na mnajua wote nini kinaendelea ndani. Wadau wa Simba tunafatilia kwa karibu hatutaki short cut!
Simba is beyond just a football club, imebeba furaha za watu na wengine hufa kwa pressure. Msicheze na kazi nzuri mliyokwisha anza na mnataka kuiharibu kwa siasa za kizamani za mitaa ya Kariakoo na twiga.