Hicho kitu kwa Sasa sioni kikitekelezeka kwa sababu zifuatazo.
1) Wakati wa magori akiwa ceo, hao umbro walikuja na dili la kwamba tuwe tunanunua jezi kwao kwa mkataba wa kwanzA..Kisha Simba waje waziuze wenyewe wakati wao wakimonitor uuzwaji wa jezi na soko, Ili mkataba wa pili waone wanaingia dili la aina Gani Kati ya kuwapa simba pesa Kisha wao wauze jezi ama waendelee na kuwauzia simba..dili hilo likafa kwa sababu Simba haikuwa tayari kutoa pesa ..( kumbuka huu ndio mfumo wa kampuni zote hapo ulizotaja zinapotaka kuingia mkataba na timu ndogo na timu za Kati katika soko la Dunia na kikanda)
2) Sababu ya pili ni kwamba mwenye tenda ya jezi za Simba kwa Sasa pia ni mkurugenzi wa bodi ya klabu, ndugu Kassim Dewji upande wa mwekezaji, so utaona ni kwa namna Gani ni ngumu yeye kuacha dili hilo, kwani kwa jinsi ilivyo yeye ni wakala wa kampuni ya uhlsports kwa Tanzania na pengine hatuwezi jua inawezekana kala dili kwa niaba ya simba Kisha akija huku anasema yeye ni msambazaji na wakala.
3) Kwa kuzingatia hoja ya kwanza, ambapo Simba haipo tayari kutoa pesa kununua jezi za hayo makampuni kwa kipindi hiki na wao wangetaka kulipwa (kwa mujibu wa magori kipindi Simba wanasign mkataba na uhlsports ) Romario LTD (Kassim Dewji) ambao ndio wasambazaji wa Uhlsports wanaipa simba pesa Kama sehemu ya udhamini , kwa mujibu wa watu wa ndani Kassim anawpaa Simba tsh 2500 - 3000 kwa kila jezi inayouzwa.
So kumalizia kwa mujibu wa hoja hizo tatu..haswa ukizingatia hoja ya pili ambapo ndani yake Kuna kaundugu ni kwamba usijeukatarajia Simba Sc itavaa jezi zingine nnje ya hizo ambazo wanavaa hivi Sasa. Ukiona wamebadilisha ujue Romarioa kaachana na Uhlsports kaamia kwa watengenezaji wengine wa jezi