Simba tunahujumiwa

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
MO please ichukue timu kimya kimya kuna viongozi wanatuhujumu kabisa. Kuna viongozi wanatuhujumu. Kuna baadhi ya viiongozi wanauza mechi sio kawaida kufungwa na African Lyon na Prison na tushinde Stand uD timu ngumu.

Simba tusimameni imara tuchukue ubingwa ile kauli ya upande wa pili ya kuwa haitatokea Simba ichukue ubingwa yawezekana inatumaliza kwa baadhi kutuhujumu.

Kocha mzuri asiguswe
 
Mmeanza kutafuta mchawi sasa. Kufunga, kudroo au kufungwa ni haki ya kila timu!
Nyie Simba vipi?
 
Yaani muwacheleweshee mishahara yao halafu wawe na morari ya kucheza kama wa kimataifa. Walipeni kwanza on time ndio mfurahie ushindi.
 
Hakuna hujuma wala nini. tumefungwa kihalali tujipange tujiandae kwa duru la pili ligi hii ngumu. Na makocha nao wabadilike watafute mbinu mbadala kwani timu nyingi sasa hivi zinapaki basi zikicheza na simba kwani wamegundua simba inacheza mpira wa kushambulia na pasi nyingi. Hivyo timu pinzani zinakuja kuzuia na kutumia counter attack. Ni jukumum la makocha wa simba nao kuja na mbinu tofauti wanapokutana na timu hizo vinginevyo simba itaisoma namba duru la pili.
 
Jiulize Yule kocha mnyasa wa Mbeya city alivyosema tumewafunga Yanga lakini ilikuwa mechi ngumu kuliko tulivyofungwa na simba.. Hata kocha wa prisons amerudia maneno hayo... Kama mpenda mpira wa miguu wachezaji wa simba hawako na nguvu na maumbo madogo inakuwa ni Kazi nyepesi kwa timu zenye kutumia nguvu sana... Na pengine walitumia nguvu zao zote kwenye mechi 13 na sasa wamechoka... Kwa mwendo huu Yanga bingwa...
 
Kufungwa mechi mbili tu ni hujuma.
Hivi mnategemea usawa huu msifungwe?
Huo utakuwa mpira wa wapi karne hii? Ule msemo kwamba mpira una matokeo matatu sio porojo, ni hali halisi!
Na bado. Vipodo vingine vinakuja bila ajizi.
 
Mpira unadunda kaka na kwenye viwanja vya ugenini ambavyo havina viwango ni changa moto kubwa kwa wachezaji
Halafu inabidi ufahamu pia kuwa timu za mikoani zinakamia sana timu za dar.
Hivyo basi acheni fikra potofu ya kutafuta mchawi.
 
Tuliza ball ww mikelele ya nn
 
Mmeanza chokochoko!

Kama Barcelona, Man City & co wanafungwa, who is Simba?!

Wachezaji huenda wamechoka, wapewe muda wa ku recover. Sio maroboti hao!
 
Huwa najisikia raha sana kila nisikiapo malalamiko aina hii na watu aina hii!
 
Kwani wanacheza Mkuu, wanauzaje Mechi??
Je, wachezaji hawapendi kushinda?

Mbona simba ikishinda hamsemi kama mnahujumiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…