Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Vigogo wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC wanatarajiwa kushuka dimbani Machi 1, 2026 katika Uwanja wa Amaan Complex kuumana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kuelekea mechi hiyo Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na alama 28 na pia wamewafunga Simba mara sita mfululizo.
Mchezo huo mkubwa wa dabi ya Kariakoo unatarajiwa kuanza saa 2:15 usiku, huku kila timu ikisaka alama tatu muhimu katika mbio za ubingwa wa ligi msimu huu.
Yanga wanaingia katika pambano hilo wakiwa vinara wa msimamo wa ligi kwa kujikusanyia alama 28 baada ya kucheza michezo 10. Kikosi hicho kimeshinda michezo 9 na kutoka sare mmoja pekee, kikionyesha ubora mkubwa msimu huu.
Kwa upande wa Simba, wao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 23 baada ya michezo 10, wakishinda michezo 7, sare 2 na kupoteza mchezo mmoja. Simba wataingia dimbani wakihitaji ushindi ili kupunguza pengo la alama dhidi ya watani zao.
Katika kumbukumbu za dabi sita zilizopita, Yanga imekuwa na rekodi bora baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yote sita mfululizo dhidi ya Simba.
Simba imefungwa michezo sita iliyopita ya 'dabi'
Simba 1-5 Yanga
Yanga 2-1 Simba
Yanga 1-0 Simba
Simba 0-1 Yanga
Yanga 2-0 Simba
Yanga 1-0 Simba
Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Nassoro Mwinchui kuwa mwamuzi wa kati wa pambano hilo. Atasaidiwa na waamuzi wasaidizi Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam na Hamdani Said kutoka Mtwara, huku Ramadhan Kayoko akiwa mwamuzi wa akiba. Mtathmini wa waamuzi atakuwa Israel Mjuni kutoka Dar es Salaam.
Mashabiki wa soka nchini wanasubiri kwa hamu dabi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na burudani ya hali ya juu visiwani Zanzibar.