Simba vs Azam, Yanga vs Azam vipi uwezo Wa Uwanja Wa Azam?

kimarabucha

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
791
Reaction score
621
Kwa mujibu Wa ratiba ya ligi kuu Simba na Yanga zitakapokuwa na mechi zao dhidi ya Azam zitacheza kwenye uwanja Wa Azam complex. Swali langu Kwa TFF je uwanja Wa Azam una weza kuingiza watazamaji wangapi? Je kama uwanja ni mdogo TFF haioni kuwa itakuwa imewakatili watazamaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwanja ni uwanja tu hata kama unaingiza mashabiki 100. Ni haki yao kuchezea uwanja wake wa nyumbani. TFF iliyopita ilikuwa inajali sana maslahi kuliko uhalisia.
 
Njooni Chamazi Acheni Kulialia, Yanga/Simba mna vitu vingi vya Kujifunza kupitia Uwanja huo. Suala la Kutazama mechi Nuua Tiketi Mapema au Angalia Luninga au Subiri mechi ya Marudiano itakayochezwa Taifa sio lazima Muende Wote Chamazi
 
Sifa kuu ya uwanja ni pitch na uzio kwa usalama wa wachezaji, hakuna sehemu yoyote duniani ambapo capacity ya uwanja ni kigezo cha kupima ubora wa uwanja kwa ajili ya michuano.
TFF wamefanya maamuzi bora sana. Uwanja ukijaa the rest wataangalia kwenye tv.
 
Watu 7,000 hata uwanja wa shule hautakiwi kuwa hivyo.

Ni dhihaka.
 
Kwani ww ulitaka washabiki wa Simba na Yanga waje wote kwan washabiki wa hizo tim huwa wanaingia wote uwanjani?

Muhimu hapo simba/yanga watacheza tu hapo Azam complex,ili nao wapate mapato ya uwanjani.

Simba na Yanga watashawishika nao kuona ni wakt wao nao kujenga viwanja vyao.

Tazama simba na yanga hawana uwanja hapo wanakosa mapato ya uwanja wao,pili simba na yanga watakapokuwa na uwanja watapata hata mapato ktk kodisha maduka yaliyopo hapo ktk mzunguko wa uwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu 7,000 hata uwanja wa shule hautakiwi kuwa hivyo.

Ni dhihaka.
Mbona mechi za kimataifa za Taifa Stars zimechezwa hapo? Acheni siasa kwenye Soka, Barcelona wana uwanja wa kuingiza watu 75,000 lakini wanaenda kucheza na timu zenye uwanja wa kuingiza watu 8,000 mpka 10,000. Tafuta taarifa uone kama timu zote za ulaya wana viwanja vikubwa.
 
Mechi za kimataifa si hoja.

Uwanja ukiwa kwapani, upo kwapani tu.

Siasa ni kung'anganiza kwamba uwanja wa watu 7,000 ambao hautoshihata kufanyia fainali za UMISHUMTA ni sawakwa timu yenye jina kubwa kama Azam.

Tataizo kubwa kabisa lililosababisha uwanja kuwa na capacity ndogo hivyoni lipi?

Bora hata wangesema watu 15,000.
 
Timu zenu za simba na yanga wanao hata huo? Au waje wacheze kwenye lile pori bunju na bwawa la lile la jangwani?
 
Nani timu yake Simba au Yanga?

Unajishebedua tu kuagua siyo?
 
Naona limekupata sawasawa!!!! Tulia dawa ikuingie
Umenipata wapi wakati unayehitaji dawa ni wewe mwenye ugonjwa wa kuzusha mambo.

Wapi nishawahi kushabikia Simba au Yanga?

Weka ushahidi hapa.

Ukishindwa wewe ndiye unaumwa ugonjwa wa kuzusha maneno bila ushahidi na inabidi upelekwe hospitali kusaidiwa.
 
Kwani ww ulitaka washabiki wa Simba na Yanga waje wote kwan washabiki wa hizo tim huwa wanaingia wote uwanjani?

Muhimu hapo simba/yanga watacheza tu hapo Azam complex,ili nao wapate mapato ya uwanjani.

Simba na Yanga watashawishika nao kuona ni wakt wao nao kujenga viwanja vyao.

Tazama simba na yanga hawana uwanja hapo wanakosa mapato ya uwanja wao,pili simba na yanga watakapokuwa na uwanja watapata hata mapato ktk kodisha maduka yaliyopo hapo ktk mzunguko wa uwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekusoma mkuu
 
Wekeni takwimu sawa, uwanja unachukua watazamaji wangapi?
 
Mtibwa nao wakomae simba na Yanga waende manungu badala ya mechi zao kuchezewa Jamhuri! Kama ni suala la 'pitch' hata ya manungu ipo vizuri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mechi za kimataifa za Taifa Stars zimechezwa hapo? Acheni siasa kwenye Soka, Barcelona wana uwanja wa kuingiza watu 75,000 lakini wanaenda kucheza na timu zenye uwanja wa kuingiza watu 8,000 mpka 10,000. Tafuta taarifa uone kama timu zote za ulaya wana viwanja vikubwa.

Hoja yako ni sawa lakini namba za idadi ya uwanja wa Barcelona, Camp Nou umekosea ni 99,354 na siyo 75,000.
 
Back
Top Bottom