Simba Vs Kagere

Sababu azam ni tawi la simba, watakaza sana mwisho watalegea. Ligi bado mtani usishangilie kabla

Hao wanajulikana kwa kuwa na matawi mengi,hasa timu zenye wamiliki wenye vinasaba vya uajemi.
 
Nasubiria matokeo ya Yanga maana hesabu zinaanza kuwa ngumu!
Tuwaombee ubaya watani wetu ili kazi iwe nyepesi
 
Hao wanajulikana kwa kuwa na matawi mengi,hasa timu zenye wamiliki wenye vinasaba vya uajemi.
Sikia ndugu...., siku hizi hapa bongo hakuna timu zenye matawi, ila kuna mamluki katika timu hizo, kwa hiyo kushinda au kushindwa kwa Azam leo kutategemea na nguvu ya mamluki itakayokuwepo kwenye starting line up yao. Mamluki ni tatizo kwenye timu hizi, kuanzia wachezaji mpaka viongozi. Timu nyingi ndogo hufa kwa sababu hii ya mamluki, hivyo ukishindwa kudhibiti mamluki huna chako kwani hata uwe na uwanja mkubwa kama Camp Nou mafanikio ni ndoto.

Hebu jiulize, Davis Mosha alikuwa mwenyekiti wa Moro United, akaiacha na kugombea umakamu mwenyekiti Yanga na kushinda, si utarudi nyuma na kujiuliza kilichomsibu Siang'a na Moro United yake, licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya poits 12, lakini mwisho haikuwa bingwa!! Nini kilifuata? Wachezaji muhimu 3 wa Mo U wakaihama timu hiyo licha ya kuwa ilipata nafasi ya uwakilishi CAF. Hiyo ndiyo nguvu ya mamluki ilivyo katika timu ndogo za bongo. Dawa yake ni kuanza kulea watoto klabuni tangia wanapoacha kunyonya na kuwafundisha mapenzi kwa timu yao ili kuwaepusha na UMAMLUKI kwa hizi timu kubwa mbili!
 
Sawa Ng'oti kuhus mamluki,lkn kuna zaidi ya hiyo.Kuwa tawi kuainvolve pia maswala ya kukatiana pochi baina yao na kundi husika ili kuibeba/kuhujumu timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…