Dakika ya 29: Mchezo umechangamka, Simba wanafanya mashambulizi kutafuta bao la kusawazisha.
Dakika ya 27: Awadhi Juma anakosa bao la wazi, anapata pasi kutoka kwa Lyanga, anaupiga kwa kichwa unatoa kidogo nje ya lango la Toto.
Dakika ya 23: Toto wanaongoza bao 1-0, Simba waliuanza mchezo kwa kasi ndogo, sasa wanaonekana kuanza kuchangamka.
Dakika ya 20: Toto wanapata bao, mfungaji akiwa ni Wazir Junior baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 likajaa wazuni moja kwa moja.
Dakika ya 19: Simba wanapata faulo nje ya 18 ya Toto upande wa kulia mwa uwanja, Kessy anapiga lakini kipa wa Toto anadaka na kuupiga mbele.
Dakika ya 16, matokeo bado 0-0, timu zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 12: Awadhi Juma anapiga shuti kali lakini linatoka nje.
Dakika ya 10: Toto wanapiga faulo lakini inapaa juu ya lango la Simba na kuwa goal kick.
Dakika ya 9 Toto wanapata faulo nje ya 18 ya Simba.
Dakika ya 8: Simba wanamiliki mpira muda mwingi ila bado hawajatengeneza nafasi.
Dakika ya 5: Timu zote bado zinasomana taratibu, mchezo haujawa na kasi kwa timu zote.
Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza.
Mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa