Simba Vs Vancouver White Caps Vipi?

Simba Vs Vancouver White Caps Vipi?

Mfumwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2008
Posts
1,455
Reaction score
42
Jamani aliye na matokeo ya Wekundu wa Msimbazi na Wakanada atupashe habari.
 
Hadi mapumziko matokeo yalikuwa Simba 1 Vouncouver 2
 
Leo Dar kulikuwa hakuna joto nini?, walipofungwa na Yebo Yebo walisema sababu ya joto.
 
Simba walala 2-1 kwa Vancouver Whitecaps wa Canada
Na Sosthenes Nyoni
TIMU ya Vancouver Whiteceps imethibisha kuwa wao ni mabingwa wa Marekani Kaskazini kwa kuonyesha kandanda safi na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Taifa.

Wamarekani hao walianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kwanza katika sekunde 55 kupitia kwa Marlon James alileunganisha vizuri krosi na kufunga bao hilo kwa kichwa na kumwachwa kipa wa Simba, Deogratias Mushi asijue la kufanya.

Baada ya bao hilo katika dakaki ya 15, Simba walifanya mabadaliko na kutoka Adam Kingwande na nafasi yake ikachukuliwa na Haruna Moshi.

Mabadiliko hayo kwa kiasi furani yalionekana kuisaidia timu ya hiyo ya Msimbazi, kwani kiungo huo wa kimataifa wa Tanzania, Haruna Moshi 'Boban' aliyefunga bao la kusawazisha katika dakika ya 23 baada ya kumlamba chenga kipa wa Whitecaps, Diego Olivera.

Wamarekani hao walipata bao la pili lililofungwa na Marlon James kabla ya Mussa Mgosi kukosa penalti kwa shuti lake kugonga mwamba na kuokolewa na mabeki wa Vancouver.

Katika jambo lisilokuwa la kawaida mashabiki wa timu ya Simba walimzomea kocha Marcio Maximo aliyekuwa jukwani na wachezaji wake wa Taifa Stars baada ya kuingia kwa Haruna Moshi na kufunga bao la kufutia machozi.
Source: Mwananchi Read News
 
Wo timu simba, yeboyebo mdebwedo sasa ona hata nafasi ya tatu tabu tupu kwa mnyama simba! Poleeeeeeeeeeeeeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Simba watani sangu eeee
 
Mh!! Kazi ipo, naanza kushangilia Azam sasa

...wala sikulaumu!

tangu napata fahamu zangu mimi mpenzi wa Simba -Taifa Kubwa, mara ya mwisho kushangilia simba ilikuwa enzi zile;

Mwameja/Iddi Pazi, Kassongo Athumani, Kassanga Bwalya, Jamhuri Kihwelu, George Masatu, Husseyn Marsha, Bakari Iddi, Ramadhan Lenny, Damian Kimti, Itutu Kigi, Mzee wa Kiminyio, Edward Chumila, Gebo Peter,...

Enzi hizo Simba, Simba kweli...TAIFA KUBWA...! tangu 1999 sijui habari zao tena

...inasikitisha sana maendeleo ya hili chama! 🙁 bora nijiliwaze na ze Gunners tu huku uzeeni!
 
Simba wameangukia pua kwa Mtibwa 1-0

Vipi watani Simba kuna nini?

Nani mchawi??
Nafasi ya Pili tutaipata tu...Mtibwa ni zuri kuliko unavyo fikilia hata yebo yebo ambae kafanya usaji wa kufuru hapa bongo anaitambua...Mungu ibariki simba iweze kupata nafasi ya kuwakilisha Taifa maana ndiyo timu tunayo iamini mechi za nje....
 
Back
Top Bottom