Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 413
Wajameni najua wengi wetu na hasa wale mashabiki wa timu hizi mbili sio siri wala nini tuko na kimuhemuhe cha kutaka kujua jinsi mpambano utakavyokuwa hapo kesho pale National Stadium..hebu wakati tukielekea kuianza week end tujadili huu mpambano wa hizi timu. Kwa mtazamo wangu naipa nafasi kubwa Simba ya kuibuka na ushindi kwa kuzingatia sana rekodi yao nzuri ya kushinda mechi 9 walizocheza ingawa hii inaweza isiwe kigezo cha moja kwa moja kwao kupata ushindi lakini kwa mtazamo wa kiutalaamu hii ndio timu bora. Yanga najua ina wachezaji wazuri ingawa kimizania hainishawishi kuipa nafasi sana ya kushinda. Najua soka ni dakika 90...Utabiri wangu Simba 2- Yanga 1