Simba Vs Yanga kesho tujadili!!!

Simba Vs Yanga kesho tujadili!!!

Status
Not open for further replies.

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
Wajameni najua wengi wetu na hasa wale mashabiki wa timu hizi mbili sio siri wala nini tuko na kimuhemuhe cha kutaka kujua jinsi mpambano utakavyokuwa hapo kesho pale National Stadium..hebu wakati tukielekea kuianza week end tujadili huu mpambano wa hizi timu. Kwa mtazamo wangu naipa nafasi kubwa Simba ya kuibuka na ushindi kwa kuzingatia sana rekodi yao nzuri ya kushinda mechi 9 walizocheza ingawa hii inaweza isiwe kigezo cha moja kwa moja kwao kupata ushindi lakini kwa mtazamo wa kiutalaamu hii ndio timu bora. Yanga najua ina wachezaji wazuri ingawa kimizania hainishawishi kuipa nafasi sana ya kushinda. Najua soka ni dakika 90...Utabiri wangu Simba 2- Yanga 1
 
UKistaajabu ya Musa utayaona ya ..... we subili kama kesho hamjatoka vichwa chini
 
Kesho rekodi inatibuliwa na watoto wa Jangwani wapo full mzuka
 
hapa kwenye hii mada ngoja niwe msomaji tu nione mashabiki watakavyo bishana
 
Kesho rekodi inatibuliwa na watoto wa Jangwani wapo full mzuka
...Fidel unajua hata yule mzungu wenu golini nadhani amepoteza confidence kabisa sijui kwa kuwa amesiki Kondic anaondoka amepata mcheche!!! Kwa kweli nina uhakika mnyama atawafanya vibaya...Invisible unasemaje Mkulu!!!
 
Na siku hizi yale mambo yenu Yanga ya kuparamia ukuta eti mnaogopa kupitia milangoni sijui safari hii mtatua na helikopta au vipi...naonea huruma sana.
 
Enzi hizo:
1-Mackenzie Ramadhani
2-Mavumbi Omari
3-Twaha Hamidu
4-Deo Njohole
5-George Masatu
6-Iddi Selemani
7-Zamoyoni Mogela
8-Malota Soma
9-Hamisi Gaga
10-John Makelele
11-Raphael Paul

Kwa hisani ya issamichuzi.blogspot
 
Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Matokeo ya kesho yatategemea nani ametoa pesa (atakayehonga) zaidi!!! Simba ua Yanga!!
 
Nemens
Mtendamema
Mkapa
Mwesa kiwelu
Kabunda
issa athuman
Sure boy
......
......
......
......
......

Simba koko anakalishwa kwenye kibao cha mbuzi huku tumemtanda ushungi, kucha zake tumempaka hina yaani mpk rrraha...
 
Homeboy pole sana.........! Kwa kiwango ambacho mnyama anakionyesha sahivi, nawapa nafasi kubwa sana Simba kuibuka na ushindi........! Poti soka la bongo si kama la Ulaya Liverpool vs Manu...Liver akiwa chini ya kiwango, kukurupuka na kumndunda Manu...hapa kwetu sio......!

Kesho homeboy (Fidel) kichapo unacho....ha!ha!ha!ha!ha!ha!aaa
 
The late Said Mwamba Kizota unforgetable heroe and star of all season, we are with u...Dar Young African Fans
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom