bemg
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 2,799
- 643
SIMBA kesho inashuka kwenye Uwanja wa Mei 8, 1945, jijini Setif, Algeria; uwanja ambao una historia ya kipekee nchini humu.
Tarehe 8, Mei mwaka 1945, majeshi ya Ufaransa iliyokuwa ikiikalia kimabavu Algeria yaliua wananchi kati ya 6,000 hadi 45,000 wa Setif katika mapambano yaliyofanyika mjini humo.
Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu 30,000 ulibadilishwa jina wakati huo na kupewa jina hilo la tarehe kwa kifaransa Stade Mai 8 1945, kwa heshima ya watu waliopoteza maisha siku hiyo.
Mauaji hayo ndiyo yaliyosababisha timu ya Setif kubadili rangi ya jezi zake kutoka nyeupe na kijana na kuwa nyeusi na kijani nyeusi ikiwa na maana ya kuomboleza maelfu hayo ya watu waliouawa siku hiyo.
simba sport club website