Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Hii ilikuwa Senegal bora kabisa iliyowahi kutokea.
Nakumbuka game ya kwanza World cup wanakutana na mabingwa watetezi Ufaransa, game inapigwa majira ya saa nane kwa saa za kwetu.
Diof anapiga cross matata kutoka kona ya kushoto, mabeki wa Ufaransa wanazembea, Barthez anapotea na Senegal wanapata goli la kwanza.
Wanakwenda kutolewa na Uturuki nakumbuka goli linafungwa na Hassan Sassi baada ya beki za Senegal kumsahau jamaa.
Hiki kilikuwa kikosi cha dhahabu.
Senegal ilikuwa na kipa bora kabisa
Kina Henry Camara
Sure!Goli la uturuki lilifungwa na ilhan Mansiz kupitia cross ya Davala (huyu jamaa alikuwa na kiduku)
baada ya haya mashindano diouf yuleeeee livapool
Ha ha na ilikuwa Gamble Garard Huellier alicheza!,matarajio makubwa kwa Diof yaliyokuwepo hayakuja...Na Liver wakamfuta kazi....baada ya haya mashindano diouf yuleeeee livapool
Anasema Stiven Gerard alikuwa anamuonea wivu, na akawa hampi ushirikiano....Jamaa alikuwa na mapafu ya mbwa, winga mmoja hatari sana ila baada ya W.cup sifa zikazidi Akaanza kuwa Bishoo , u Africa ulimuathiri mpira ukamshinda .
Anasema Stiven Gerard alikuwa anamuonea wivu, na akawa hampi ushirikiano....
u have good memory bro!nakikumbuka Sana hiki kikosKocha wa hiko kikosi alikuwa Marehemu Bruno Metsu.
Hapo kikosini nawakumbuka golikipa Tony Silva, Captain Aliou Cisse ambaye kwasasa ndiye kocha mkuu wa kikosi hiko, pia Ferdinand Coly huyo jamaa mwenye rasta.
Kiungo matata kabisa aliyestafu mpira mapema kutokana na matatizo ya moyo, Khalilu Fadiga mwenye jezi namba 10.
Pia kuna Salif Diao namba 15, Henry Camara mwenye namba 7, Beki ya kulia Omar Daf mwenye namba 2.
El Hadji Diouf mwenye 11, na Papa Bouba Diop mwenye 19 ambaye aliwagunga Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia.
Pia walifungwa na Cameroon katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2002 kwa mikwaju ya penati.
Miaka ya 2000 ilikuwa ni wakati mzuri kama mshabiki wa soka kufatilia soka kutokana na uwepo wa kikosi kama hiki.
Ahsante mtoa mada kwa kutukumbusha mbali.
cc: Guasa Amboni
Thanx brou have good memory bro!nakikumbuka Sana hiki kikos
Pia alikuwa mtukutu sana ndani na nje ya uwanjaJamaa alikuwa na mapafu ya mbwa, winga mmoja hatari sana ila baada ya W.cup sifa zikazidi Akaanza kuwa Bishoo , u Africa ulimuathiri mpira ukamshinda .