njaakalihatari
JF-Expert Member
- Feb 12, 2019
- 4,081
- 8,671
Mashabiki hao mara baada ya kufika hapa hotelini saa 11:10 jioni kwa saa za Kinshasa walianza kuimba nyimbo zao mbalimbali.
Wakiwa wanaimba nyimbo hizo walikuwa wakipiga jengo la hoteli ambao walikuwa wamefikia Simba.
Hawakutaka kumuona mtu yoyote ambaye hawapo nao anapita katika eneo hilo zaidi ya wao kufanya vurugu ikiwemo kupigana.
Mmoja wa wahudumu ambaye ni Mkongomani alikutana na kadhia ya kupokonywa simu na mashabiki hao akiwa anawarekodi.
Walinzi wa hoteli hiyo walishishirikiana kwa pamoja kuwazuia kuna muda walifanikiwa wakati mwingine walionekana kushindwa.
Baada ya kufanga vurugu mbalimbali nje ya hoteli hiyo ya Simba waliondoka wakiwa na pikikipi zao huku wakiwa wanaimba.
Kuna mashabiki walioshika silaha kama fimbo na walikuwa wanapigana na kuwapiga watu wengine.
Kuna ambao walikuwa wanaonyesha ishara mbalimbali kama ile ya kunyonga
Muda mfupi baada ya mashabiki wa AS Vita kuvamia hoteli ya Royal waliyofikia Simba mjini Kinshasa, leo Februari 12, 2020 winga wa timu hiyo, Bernard Morrison alitaka kuzichapa nao.
Morrison alitoka mlangoni akionyesha nia ya kuwafuata ila alizuiwa na walinzi wa hotel pamoja watu waliokuwa karibu nae.
Hata hivyo alirudishwa ndani ya hoteli na kutulizwa asifanye chochote na kutulia.
Simba imeanza msafara wa kwenda Uwanja wa Stade Des Martyrs kwa ajili ya mtanange wa hatua ya makundi CAF dhidi ya AS Vita utakaoanza saa 4 kamili usiku.