Kwenye hii video Manara anadai kuna Fact ambayo haisemwi kuwa Simba ilianza kuuza jezi na tiketi wiki 5 nyuma.
Yanga wametumia wiki 1 tu kuuza tiketi na jezi na zimeisha, huku akisema kuna propaganda ambazo yeye alikuwa anatumia huenda ndio Simba wametumia kuonesha wamemaliza tiketi zao( Sold out)
Anesena wana Yanga wajipongeze kwa kumaliza tiketi hizo kihalali.
Je, Ni kweli Simba walianza kuuza Tiketi wiki 5 nyuma? Jamiicheck naomba msaada hapa tupate ukweli.
Yanga wametumia wiki 1 tu kuuza tiketi na jezi na zimeisha, huku akisema kuna propaganda ambazo yeye alikuwa anatumia huenda ndio Simba wametumia kuonesha wamemaliza tiketi zao( Sold out)
Anesena wana Yanga wajipongeze kwa kumaliza tiketi hizo kihalali.
Je, Ni kweli Simba walianza kuuza Tiketi wiki 5 nyuma? Jamiicheck naomba msaada hapa tupate ukweli.
- Tunachokijua
- Simba Sports Club ni klabu ya soka yenye makazi yake katika kata ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania.
Simba Ilianzishwa mwaka wa 1936, Jina la utani ni Wekundu wa Msimbazi (Wekundu wa Msimbazi), ni kumbukumbu ya watani wao wote wenye wekundu hao na Mtaa wa Msimbazi uliopo Kariakoo yalipo makao makuu yao.Simba nin moja ya klabu yenye Wingi wa mashabiki na moja kati ya klabu kubwa nchini Tanzania.
Mnamo Agosti 2, 2024 kwenye Kipindi cha Jana na leo cha Wasafi FM alisikika Haji Manara akidai kuwa Klabu ya Simba walianza kuuza jezi zao za msimu mpya wa 2024/2025 pamoja na tiketi za Tamasha la Simba Day wiki tano nyuma.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa kauli hii haina ukweli kwani Pitio letu katika kurasa rasmi za SimbaSC za mtandao wa Instagram na X zinaonesha Simba walianza kuuza tiketi zao Julai 22, hadi Julai 31 2024 sawa na siku 11 na ikiwa ni siku 12 nyuma tangu Haji kutoa kauli hii Wakati Yanga walianza kuuza tiketi Julai 19 hadi Agosti 02, 2024 sawa na siku 15.
Chapisho la Simba kutoka mtandao wa X ikionesha kuanza kuuzwa Tiketi Julai 22 2024
Chapisho la Yanga kutoka mtandao wa X likionesha kuanza kuuzwa kwa tiketi Julai 19 2024
Pia, JamiiChek imefanya mawasiliano na Meneja wa Oparesheni wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), Nasra Mugheri ambaye amesema, Tiketi za Simba na Yanga zilianza kuuzwa tarehe ambayo walitangaza kwenye mitandao yao ya Kijamii, kabla ya hapo hakukuwa na Mauzo ya tiketi hizo
Meneja wa Oparesheni wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), Nasra Mugheri amesema:
Tiketi za Simba zilianza kuuzwa tarehe ambayo Simba walitangaza kwenye mitandao yao ya Kijamii, kabla ya hapo hakukuwa na Mauzo ya tiketi hizo.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Yanga, nao tiketi zilianza kuuzwa siku ambayo walitangaza kwenye mitandao yao ya Kijamii
Aidha, kuhusu mauzo ya jezi za Simba ufuatiliaji wetu umebaini kuwa, uzinduzi rasmi wa jezi na mauzo kwa mashabiki ulianza Julai 24, 2024 ikiwa ni siku 10 kabla Haji kutoa kauli hii.