kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Baada ya kukikagua kikosi chao na kile cha Yanga, Simba walijua kuwa hawako tayari kucheza derby na kufungwa tena na yanga kwa mara ya 5 mtawalia, ila hawakujua wataanza vipi kuacha kupeleka timu uwanjani siku ya mechi. Baada ya kutafakari sana wao wenyewe na kuwasiliana na baadhi ya wajumbe walioko kwenye bodi ya ligi ambao ni Simba allies, ndiyo wakaja na mpango huu wa kwenda uwanjani usiku bila kutoa taarifa pahala pooopooote pale ili wakute jambo litakalowapatia sababu (nyepesi) ya kugomea mechi.
Baada ya kukuta geti la uwanja limefungwa hawakutaka kuhangaika na kupata maoni na ushauri kutoka uongozi wa uwanja (BMT, Wizara), TFF/Bodi ya ligi wala vyombo vya dola (kamanda wa polisi Dar) ingawa uwezo wa kufanya hivyo walikuwa nao. Hawakutaka kupata maoni ya watu hao kwasababu wangesababisha geti lifunguliwe na kukosa hoja ya kugomea mechi.
Ingawa kanuni ipo ya kuruhusu timu ngeni kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi siku moja kabla ya mechi lakini kanuni hii kwa hapa kwetu Tanzania ni optional; sio mandatory (lazima) kwamba lazima timu zote kwenye ligi zifanyike mazoezi ya mwisho la sivyo mechi itaahirishwa. Kwanini simba mara hii waliigeuza kanuni hii kuwa ni mandatory (pre-requisite) ya kucheza mechi na Yanga tarehe 8?, Je, Simba huwa mechi zake zoooote ilizocheza huko nyuma zimetanguliwa na kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mazoezi kabla ya mechi? Kama sio, kwanini iwe ni lazima safari hii kwenye mechi hii?
Kulikuwa na dhamira (maandalizi) ya Simba kugomea kupeleka timu uwanjani. Yanga ipewe points zake 3 na simba lolote liwakute kwa mujibu wa kanuni za ligi na sheria za nchi kwa walioathirika na uwahirishwaji wa mechi.